Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:19 am

RAIS RAMAPHOSA: JUMATATU SIKU YA KUZUNGUMZA KISWAHILI AFRIKA KUSINI

Dar es Salaam. Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema anafanya jitihada kubwa kujifunza lugha ya Kiswahili kupitia vitabu alivyopewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli wa Tanzania na ametenga siku ya Jumatatu kuwa siku rasmi ya kuzungumza kiswahili.

“Jana nilimwambia Rais Magufuli kuwa nimejifunza Kiswahili kwa kiasi kikubwa kupitia vitabu alivyonipa na nimekuwa nailewa sana lugha hiyo ila kwa kuwa tuna lugha 11 nchini Afrika Kusini, nimeitenga siku ya Jumatatu kuzungumza Kiswahili. Hivyo kama unataka kujua ni kiasi gani naweza kuzungumza Kiswahili tukutane Jumatatu,” ameongeza

Rais Ramaphosa yupo nchini tangu juzi Jumatano Agosti 14,2019 kwa ziara ya siku mbili kisha kesho Jumamosi atakuwa miongoni mwa wakuu wa nchi watakaoshiriki Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Pia Rais huyo ametoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao katika ajali ya lori la mafuta ya petroli mkoani Morogoro Jumamosi iliyopita Agosti 10,2019 ambapo hadi jana vifo vilivyotokana na ajali hiyo ni 89 na majeruhi zaidi ya 30 wakiendelea kupatiwa matibabu.

Akizungumza leo Ijumaa Agosti 16,2019 katika kituo cha Mazimbu mkoani Morogoro Rais Ramaphosa amesema harakati zake za kujifunza Kiswahili zilianza Mei 2019 baada ya kutembelewa na Rais Magufuli.

Amesema uhusiano wake na Kiswahili umeanza kujengeka kuanzia muda huo na anaendelea kufanya jitihada ili aweze kuimudu lugha hiyo.

“Rais Magufuli alikuja Afrika Kusini na kunialika nije Tanzania, nilikubali. Pia alinitaka nijifunze Kiswahili na akanipa vitabu nikaanza kusoma na kujifunza kuanzia Mei, Juni, Julai na sasa ni Agosti,” amesema Rais Pamaphosa.