- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RAIS MKAPA : WALITAKA NIBADILISHE KATIBA, VIWE VIPINDI 3 VYA URAIS
Mwanza. Rais wa awamu ya tatu, nchini Tanzania Benjamin Wiliam Mkapa amesema kuwa baadhi ya wazee wa Zanzibar walimfuata na kumshawishi aruhusu mabadiliko ya katiba ili kumwezesha aliyekuwa Rais wa Zanzibar kwa wakati huo kuongoza kwa mihula mitatu badala ya mbili za kikatiba.
Siri hiyo aliitoa juzi jijini Mwanza wakati wa hafla ya kutambulisha kitabu chake, Mkapa alisema suala hilo lilikuwa kiunzi ambacho kilikaribia kumuingiza kwenye mtikisiko kiuongozi.
“Nilikaribia kupata mtikisiko lakini nilifanikiwa kuruka kiunzi hicho ingawa ilikuwa kazi nzito kweli. Tulizungumza kwa makini na hatimaye tulielewana; na katiba ya Zanzibar ikabaki na vipindi viwili vya miaka mitano kama ilivyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano,” alisema
Alisema kufanikiwa kuruka kiunzi hicho ni miongoni mwa mambo anayojivunia na kuona ufahari kwa sababu aliweza kulinda Katiba ya Zanzibar na ile ya Muungano hadi alipokabidhi kijiti cha uongozi kwa Rais Jakaya Kikwete.
Alisema anafurahi kuona msingi wa uongozi unaolinda na kuheshimu katika kupokezana vijiti unaendelea kuheshimiwa na viongozi waliofuata baada ya Kikwete naye kumkabidhi kijiti Rais John Magufuli.
Mungu ampe (Magufuli) afya njema aongoze awamu mbili (ya miaka mitano mitano kwa mujibu wa katiba); nina hakika hatataka kuongeza awamu ya tatu,” alisema Mkapa.
Alitumia nafasi hiyo kuelezea jinsi alivyomteua na kumwingiza Rais Magufuli katika baraza lake la mawaziri huku akimmwagia sifa kwa uchapa kazi aliouonyesha na ameendelea kuonyesha hata sasa akiwa rais.
“Nilipounda Baraza la Mawaziri nililolipachika jina la “Askari wa mwamvuli” John Magufuli alikuwa miongoni mwao akiwa (naibu) waziri wa ujenzi alikoleta mabadiliko makubwa. Watu wa Kusini hawatamsahau kwa ujenzi wa Daraja la Mkapa pale Mto Rufiji ambalo kwa kweli lilistahili kuitwa Daraja la Magufuli,” alisema Mkapa