- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RAIS MAGUFULI: WATANZANIA MSIFICHE PESA NJEE YA NCHI HATAKAMA NI ZAWIZI
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewataka Watanzania kuwekeza nchini na kuachana na tabia ya kukimbizia fedha zao nje ya nchi kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia wengine kufaidika na uwekezaji huo bila kujali kama waliiba fedha hizo au la.
Kauli hiyo ya Rais ameitoa leo Januari 11, 2020 alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari Mwanakwerekwe iliyopo Mjini Magharibi na Hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Hotel Verde Azam Luxury Resort and Spa iliyopo Mtoni Unguja wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi visiwani Zanzibar.
“Viongozi ndani ya serikali zote mbili pamoja na wananchi wanaotaka kuwekeza wasiogope, ninafahamu wapo watanzania wenye fedha nyingi lakini wanaogopa kuwekeza hapa nchini badala yake wanaenda kuwekeza nje siku mkifa hizo fedha zitaliwa huko huko.
“Wenye fedha zao wawekeze hapa kwani kwa kufanya hivyo unajenga mazingira mazuri ya watu wengine kufaidika na uwekezaji wako hata kama uliiba lakini zitasaidia watanzania wengine tumeambiwa hapa wametengeneza ajira za watu zaidi ya 200 na hawa walioajiriwa kwanza wanamuombea mzee Bakhresa kwasababu wameimarika kiuchumi.
“Niwaombe sana watanzania pamoja na wanasiasa wenzangu msiogope kuwekeza, msifiche mali zenu hata kama mlizipata kiuficho mziachie wazi zikafanye kazi za watanzania, mzee Bakhresa endelea kuwafundisha watanzania wengi namna ya kuwekeza kwa manufaa ya nchi yetu,” amesema Rais Magufuli.