- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RAIS MAGUFULI: TULIPIMA MAPAPAI, FENESI, MBUZI TUKAKUTA VINACORONA
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameonesha kuwa na mashaka na matokeo ya vipimo vya maabara ya taifa ya Dar es salaam juu ya vipimo vya ugonjwa wa Corona, mara baada ya kupeleka sampuli ya vitu mbalimbali ikiwemo Mbuzi, fenesi, Papai, Kondoo na Oili ya magari kwa ajili ya kuvipima na kujua ukweli wa Matokeo ya maabara hiyo.
"Tulichukua sampo za Mbuzi , Kondoo, Papai,Oili ya magari na sampo nyingine za vitu mbalimbali na kisha kuvipeleka kwenye maabara ya Taifa kwa ajili ya kuvipima.Tulifanya hivyo bila wao wao kujua na tukazipa majina .
"Sampo ya oil kwa mfano iliyotoka kwenye gari ilipewa jina la Jabir Hamnza(30) , ile ilileta matokeo haina Corona,tulipopeleka sampo ya Fenesi ambalo lilipewa jina la Sarah Samweli(45)matokeo yalionesha kuwa na Corona, tulikopeleka sampo ya Papai na kupewa jina la Elaberth Anne( 26) matokeo yalionesha Papai lina Corona,"amesema Rais Magufuli.
Amefafanua maana yake ni maji ya mle ndani kwenye Papai yana Corona na kuongeza walipeka sampoya ndege Kware matokeo yake naye akawa na Corona, walipeleka sampo ya Mbuzi akawa na Corona , wakapeleka Kondoo akawa hana Corona.
"Sasa tukishaona umepeleka sampo ukamwambia huyu ni binadamu halafu ikaleta matokeo ya kuwa na Corona maana yake mapapai yote yangewekwa katantini, ukipelekea sampo ya Mbuzi na ukaambiwa ana Corona maana yake mbuzi zote nazo ziwe karantini.Ukipeleka fenesi likawa positive , hivyo mafenesi nayo yalitakiwa kuwa karantini.
"Ukishagundua kitu kama hiki lazima ujue kuna mchezo wa ajabu unafanyika kwenye vipimo hivyo, kuna mambo ya ajabu yanafanywa katika nchi hii, aidha wahusika wamenunuliwa au hawana utalaam jambo ambalo sio kweli kwani maabara hiyo imekuwa ikitumika sana kwenye magonjwa mengine.
"Aidha zile sampo zilizopelekwa kwasababu kila kitu kinatoka nje, hadi vile vipamba vinatoka nje, hivyo lazima kuna kitu fulani kinafanywa na kama mapapai nayo yanaonekana positive yana Corona basi WHO inatakiwa kufanya kazi kubwa katika hili,"amesema Rais Magufuli.
Ameongeza kama hali ndivyo ilivyo basi kua uwezekano mkubwa wanasayansi hawajafanya tafiti za kutosha katika hilo, kwa hiyo kuna watu kutokana na mazingira ya aina hiyo huenda wameambiwa wana Corona wakati hawana.
"Inawezekana wengine wakafa kwa hofu wakati Papai lile lipo linaiva, Mbuzi yupo hajafa , Fenesi lipo labda lije lioze tu baadae kwa muda wake.Fenesi lipo kwasababu halisikii huenda lingekuwa linasikia nalo muda huu lingeshaoza.Kwa hiyo natoa mwito kwa Watanzania msiwe na hofu na hasa kwa wale ambao hawajachoka wala kuumia,"amesema Rais Magufuli.
Pia amesema lazima kuwe na maswali mengi ya kujiuliza kama Tanzania, Afrika na Dunia huku akisisitiza huenda kuna kitu fulani hakijafahamika kwa Watanzania, na kwa wanasayansi na inawezekana hata duniani hawajakielewa.Hivyo ametoa mwito kwa wale wanaotumia vifaa hivyo kwa Afrika wachukue sampo za wanyama au hata za kitu chochote hata likuta, mjusi, wachukue chochote , watakuja kuthibitisha hayo anayozungumza.
"Mimi ni mwanasayansi,najua ninachozungumza, na kazi hii imefanywa na watu wenye ujuzi wa hali ya juu.Narudia kuwaambia Watanzania tusipaniki tuendelee kuchapa kazi, uzalishaji uendelee, tusitishane na wanasiasa waache kuchukua hii kama ajenda haitawasaidia
"Mtu anazungumza funga Dar es Salaam, funga Tanga, sifungim nilishasema sifungi na sitafunga.Tuchape kazi na tuendelee kuchukua tahadhari.Sasa wewe kama Waziri wa Katiba na Sheria nenda kashiriane na Wizara ya Afya kuangalia kwenye hiyo maabara kuna nini ndani.
"Kama kuna kitu kama Criminal basi kishughulikiwe kwa mujibu wa sheria, kama kuna watu walijihusisha kufanya Criminal kwa kutumia hivyo vifaa basi sheria ichukue mkondo wake, na kama vifaa hivyo vinatatizo kiufundi basi navyo viangaliwe,"amesema Rais Magufuli.
Aidha Mh Rais Magufuli amerejea kauli yake ya kuwataka Watanzania kutokuwa na hofu kubwa dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19) na badala yake waendelee kuchukua tahadhari kama zinavyoelekezwa na wataalamu.
Rais ametoa kauli hiyo wakati akimuapisha Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, hafla iliyofanyika wilayani Chato, mkoani Geita.
Amefafanua kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa ambao unasambazwa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii na kusababisha hofu kubwa kwa wananchi, hali ambayo haisadii kupunguza tatizo bali kuliongeza na kutengeneza sintofahamu kubwa.
Amewataka Watanzania wote hasa wanasiasa pamoja vyombo vya habari kuacha kueneza taarifa zinazowajaza watu hofu ama kutumia ugonjwa huu kwa manufaa ya kisiasa na badala yake waungane kutoa elimu sahihi na kuhimizana kuchukua tahadhari za kutoambukizwa.
Ameelezea kushangazwa kwake na viongozi ambao wanazuia watu wanaofariki dunia kusafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao, na Viongozi wa Dini walioonesha kutetereka kiimani, hivyo ametoa wito kwa viongozi wote kusimama imara, kuonesha uongozi wa kweli na kuwapa matumaini wananchi badala ya kuwajaza hofu.
Katika uapisho huo, Rais Magufuli amemtaka Nchemba kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa na mtangulizi wake Marehemu Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga aliyefariki dunia tarehe 01 Mei, 2020 na pia kushirikiana na viongozi wenzake katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya Serikali.
“Nimekuteua kwa mara ya pili kwa sababu naamini unaweza kutekeleza jukumu hili vizuri, na bahati nzuri vijana wengi niliowateua hawajaniangusha, kwa hiyo nakutakia heri katika kazi zako na Mungu akutangulie,” amesema Rais Magufuli.