Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:57 pm

RAIS MAGUFULI : MSONGAMANO WA MAGEREZANI WENGI NI KESI ZA KUSINGIZIWA

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kuwa kwenye Magereza mengi nchini kumekuwa na Msongamano mkubwa wa mahabusu na wafungwa kwasababu ya viburi na jeuri ya Matajiri kuwaweka watu ndani kwa sababu ya Pesa zao na wengine kwa sababu ya Kesi za Kusingiziwa.

Kauli hiyo ameitoa leo Februari 6, 2020 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria

"Kuna msongamano kwenye magereza zetu, wengine kesi zao ni za kusingiziwa au wengine wako mahabusu wanateseka kwasababu ya Matajiri kusema ‘ nakukomesha utakaa mahabusu’, Wapelelezaji nao kila siku upelelezi unaendelea tena kwa makusudi msipotubu ufalme wa Mungu itakuwa vigumu kuuona”

"Ndani ya siku mbili tatu nitasaini hati ya kuwarudisha makwao wafungwa ambao ni raia wa kigeni, Wakimeo Raia wa Ethiopia 1415, hii itasaidia pia kupunguza msongamano kwenye Magereza zetu, naambiwa mahabusu ni wengi kuliko wafungwa"- JPM

“Kuna changamoto ya dhuluma kwa Wanawake hasa wajane na migogoro ya ardhi, sina hakika kama Mabaraza ya ardhi yanafanya kazi vizuri pengine yapo chini ya Wizara ya Ardhi, lakini wanapoharibu lawama zinarudi kwa Mahakama" - JPM

“Jaji Mkuu uangalie namna bora ya uendeshaji wa Mabaraza ya ardhi. Wakati nikiwa Waziri wa Ardhi nilishaandaa majina ya watendaji wa Mabaraza waliotakiwa wafukuzwe, inawezekana bado wapo huko”