Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 4:43 pm

RAIS MAGUFULI "MAJUNGU HAYAJENGI, NAWAAMBIA NDUGU ZANGU KWA DHATI KABISA"

Dar es salaam: Rais John Magufuli, amewataka wananchi na wanaccm kuacha tabia ya kufanyiana majungu, huku akisema kuwa majungu yanachelewesha kwenda mbele kwasababu hayajengi.

Kauli hiyo ya Rais Magufuli ameitoa Jana May 2, 2019 baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa njama za kumchefua Mbunge wa Mbarali, Haroub Mohamed (CCM), zikiwamo kuwekewa bunduki kwenye shamba lake kwa lengo la kumchafua.

“Changamoto nyingine iliyopo Mbarali ni majungu, mtaichelewesha kwenda mbele, ninajua wapo watu ambao wamelipwa hela, wamepangwa kuja kumzomea mbunge, haya hayatawasaidia, ukiwa unataka ubunge, usububiri wakati, subiri uje umshinde kwenye kula, lakini haya majungu yanawachelewesha," alisema.

"Majungu hayajengi, ninawaambia ndugu zangu kwa dhati kabisa, mnapochagua watu hamchagui malaika, huyu ni mbunge wa kuwatumikia watu, mmepanga kumchafua, hatachafuka.

Vilevile, amesema mbunge huyo ameundiwa kundi la watu ambao wanalipwa pesa na watu wenye nia ovu dhidi yake. Rais Magufuli alifichua njama hizo jana katika mkutano wa hadhara alioufanya katika Viwanja vya Rujewa wilayani Mbarali ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Mbeya.

"Mmefanya mengi ya ajabu, mkaenda kwenye shamba lake mkaenda kufukia silaha ambazo wala siyo zake kwa umiliki, msifikiri hatujui, acheni mambo ya namna hiyo na bahati nzuri wanaofanya hayo wanajulikana, kama hizo ndizo mbinu za kupata ubunge hupati, mimi ndiyo mwenyekiti." Rais Magufuli pia aliaziga apewe majina ya watu waliopewa hekta 5,900 ambazo serikali iliagiza zirudishwe kwa wananchi kutoka kwa wawekezaji.

"Haiwezekani wananchi wote wa Mbarali mimi nimetoa ardhi halafu wao walalamike kwamba hawajapata ardhi wakati mimi nimetoa, isije ikawa zimerudi tena kwa wawekezaji au wamekuja wengine wapya kisirisiri. "Lengo la yale mashamba yalikuwa si kupewa wawekezaji tena, lengo lilikuwa ni kupewa wananchi kwa ajili ya kulima," Rais Mgufuli alisema.