November 26, 2024, 10:45 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RAIS MAGUFULI: LEO NIMEONA MPIRA, SIO ULE WA SIKU ZA NYUMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kufuzu kucheza fainali za michuano ya Afrika (AFCON 2019). Mhe. Rais Magufuli ambaye alikuwa akifuatilia pambano hilo kupitia Luninga amerekodiwa picha ya video akifurahia ushindi baada ya pambano la Taifa Stars na Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) kumalizika kwa Taifa Stars kupata ushindi wa Magoli 3 kwa 0
"Leo nimefurahi sana, mpira huu tulivyoshinda hivi. Sasa angalau Taifa Stars wameipa heshima nchi yetu, leo nimeona mpira, si ule wa siku za nyuma. Ndio maana mimi sikutaka kwenda kabisa niuangalie hapa" amesema Rais Magufuli
Mhe. Rais Magufuli amesema ushindi huo ni heshima kubwa kwa nchi na amewapongeza wachezaji na Watanzania wote kwa kufanikiwa kupeleka Timu yao ya Taifa katika fainali za AFCON ikiwa ni miaka 39 tangu ilipofanikiwa kufika hatua hiyo mwaka 1980.
Mchezo wa Taifa Stars na The Cranes umefanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Machi, 2019