- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RAIS MAGUFULI AZIPA SIKU 5 WIZARA ZA FEDHA NA UCHUNGUZI KUACHIA VIFAA BANDARINI
RAIS John Magufuli ametoa siku 5 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango, kuhakikisha vifaa vya ujenzi wa chelezo ya kujengea meli vilivyokwama bandari ya Dar es Salaam kwa sababu ya kodi, vinaachiliwa na kufika mwanza mara moja kabla ya tarehe 20 mwezi huu.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo alipotembelea Bandari ya Mwanza, kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chelezo, ukarabati wa meli 5 na ujenzi wa meli mpya katika Ziwa Victoria, unaogharimu zaidi ya Sh. 150 Bilioni, unaofanywa na kampuni 2 kutoka nchi ya Jamhuri ya Korea.
Rais Magufuli ameagiza wizara ya fedha iliyo chini ya Dk. Phillip Mpango na Wizara ya ujenzi iliyo chini ya Isack Kamwelwe, kuhakikisha vifaa hivyo, ikiwemo na vifaa vya ukarabati wa meli, vilivyokwama kutokana na mchakato wa kikodi vinafikishwa katika Bandari ya Mwanza.
Aidha, Rais Magufuli amekasirishwa na ucheleweshwaji wa makontena 58 yenye vifaa vya ujenzi vilivyoagizwa na kampuni ya ukandarasi za Korea Total Marine Innovation (KTMI) na STK JV Saekyung Construction Ltd za Korea, kwa kusubiri msamaha wa kodi. Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagiza mitambo miwili ya kunyanyulia mizigo iliyokuwa imeuzwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kurejeshwa mara moja.