- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RAIS MAGUFULI AMTAKA KAMANDA MULIRO KUSHUGULIKIA KESI ZISIZO NA MASHIKO
Mwanza: Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro, kushugulikia kesi ambazo hazina mashiko huku akitoa ahadi kuyafanyia kazi malalamiko ya kero alizopewa na wafungwa wa gereza la Butimba huku akiwataka wakuu wa gereza hilo kutowasumbua wafungwa waliotoa kero zao.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 16, 2019 alipotembelea gereza la Butimba na kupata fursa ya kusikiliza kero wanazokutana nazo wafungwa na mahabusu hao ambapo amewataka maofisa wa polisi wa gereza hilo kutowaadhibu kwa kuuliza na kutoa maoni yao na kwamba iwapo watafanya hivyo wasijutie hatua atakazozichukua juu yao.
“Mkuu wa magereza hawa watu wote waliotoa kero zao hapa wasisumbuliwe asitokee mtu akawauliza kwanini waliuliza swali na wakaanza kusulubiwa na ninataka niwaambie nitajua na nikijua msinilaumu kwa maagizo nitakayoyatoa,” amesema Rais Magufuli.
“Kufungwa au kuwa mahabusu haimaanishi kuwa hauna haki ya kupata utu wako ndio maana nimekuja hapa kuwasalimu, nimesikia changamoto zenu na za maaskari wangu nao wanafanya kazi katika mazingira magumu ninajua kuna waliofungwa ambao hawajafanya makosa na ninajua kuna waliokaa mahabusu wanacheleweshewa kesi zao ili wasipate kazi za au kwasababu hawajazungumza vizuri na polisi,” amesema.
“Mkuu wa magereza hawa watu wote waliotoa kero zao hapa wasisumbuliwe wala asitokee mtu akawauliza kwanini waliuliza swali na wakaanza kusulubiwa na ninataka niwaambie nitajua na nikijua msinilaumu kwa maagizo nitakayoyatoa, nimekuja kwa wapiga kura wangu na siku nyingine nitakuja tena,” amesema.
“Niliyoyaona yamenigusa mimi ni kiongozi wenu lakini pia ninamuogopa Mungu hivyo ninawaomba mvumilie na nimekuja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, RPC ambaye yeye ndiye msimamizi wa polisi wote katika Mkoa huu, kamati ya ulinzi na usalama, wanajeshi saa ninachowaahidi ni kwamba nimewasikia sasa mniache nikayafanyie kazi,” amesema.