Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 12:55 pm

RAIS BIDEN ATAKA KUTATHIMINI UPYA UHUSIANO WA MAREKANI NA SAUDIA

Rais wa Marekani Joe Biden anataka "kutathmini upya" uhusiano wa Marekani na Saudi Arabia, Ikulu ya Marekani imesema siku ya Jana Jumanne. Kauli hiyo linafuatia kutokana na tatatizo la kidiplomasia baada ya Wazlishaji wakubwa wa mafuta Duniani OPEC kufanya uamuzi wa kupunguza viwango vyake vya uzalishaji wa mafuta duniani, uwamuzi ambao utainufaisha zaidi Urusi kukwepa vikwazo vya nchi za Magharibi na Marekani.

US President Biden arrives in Saudi Arabia, meets MBS | Daily Sabah

Mnamo mwezi wa Julai, rais wa Marekani alikwenda Riyadh kukutana na mwana mfalme ambaye aliapa nchi yake kuendeleza uhusiano na Marekani, lengo kuu la safari yake ile ilikuwa kumshawishi mwanamfalme kuongeza uzalishaji wa mafuta Duniani ili kupunguza nafasi ya Urusi kuuza mafuta yake baada ya nchi za Magharibi na Marekani kumuwekea vikwako.

Athari ya moja kwa moja ya udhalilishaji wa kidiplomasia aliyopata Joe Biden wiki iliyopita, kupeana mkono na Mohamed ben Salman ambako ilitafsiriwa kuwa alipigwa kofi usoni, kama vyombo vya habari vya Marekani vinavyoandika.

wiki iliyopita, OPEC+ ilitangaza kwamba itapunguza uzalishaji wake wa mafuta. Kashfa kwa Ikulu ya Marekani ambayo inajibu leo. "Rais amekuwa wazi, alisema msemaji wake John Kirby, lazima tutathmini upya uhusiano huu" na Saudi Arabia. Naye Joe Biden anasema yuko tayari kutafakari upya uhusiano huu kwa ushirikiano na Congress, wakati ambapo maafisa kadhaa waliochaguliwa wenye ushawishi mkubwa wanatoa wito wa kukomesha kuiuzia silaha ufalme wa Saudi arabia.

Kundi hililinajumuisha nchi 13 wanachama wa Opec (Shirika la nchi zinazouza mafuta), ambazo ni pamoja na nchi za Mashariki ya Kati na Afrika. Ilianzishwa mwaka wa 1960 kama chombo maalum, kwa lengo la kudhibiti usambazaji wa mafuta na bei yake kote duniani.

Siku hizi, mataifa ya OPEC yanazalisha 30% ya mafuta ghafi duniani, takriban mapipa milioni 28 kwa siku. Mzalishaji mkubwa wa mafuta ndani ya Opec ni Saudi Arabia - ambayo inazalisha zaidi ya mapipa milioni 10 kwa siku.

Mwaka 2016, wakati bei ya mafuta ilikuwa chini, OPEC iliungana na wazalishaji 10 wa mafuta wasio wa Opec kuunda Opec+.

Miongoni mwao Urusi, ambayo pia inazalisha zaidi ya mapipa milioni 10 kwa siku.

Kwa pamoja , nchi hizi zinazalisha karibu 40% ya mafuta yote ghafi dunia.