- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
PROF LIPUMBA: MIMI NAUNGA MKONO VIJANA WAKIJIFUNGUA KURUDI SHULE
Dar es salaam. Mwenyekit wa chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahimu Lipumba amesema kuwa yeye anaunga mkono kwa dhati swala la Mabinti wa kitanzania wanaopata ujauzito kurudi mashuleni mara tu baada ya Kujifungua.
Amesema kuwa swala la msingi ni Serekali kuweka kwanza mazingira ya kuwalinda vijana wa kike wasipate ujauzito tangu mwanzo.
“Mimi naunga mkono vijana wakiwa wajawazito wakijifungua warudi shule ila kwanza tujenge mazingira wasipate ujauzito tangu awali ila ikitokea wapate fursa ya kurudi shule” Mwenyekiti CUF, Ibrahim Lipumba
Kauli hiyo ya Prof Lipumba ameitoa leo Machi 16, 2020 wakati akifanyiwa mahojiano na ofisi za Mwananchi Tabata jijini Dar es salaam
Prof. Lipumba amesema pia licha ya kuunga mkono suala la Vijana kurudi shule lakini amepinga vikali kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kwenda kuishtaki Serekali ya Tanzania kwa Benki Kuu ya Dunia mpaka kupelekea nchi kunyimwa mkupo na Benki hiyo uliokuwa unakuja kwenye miradi ya elimu nchini.
Kitendo hicho Prof. Lipumba amekiita kuwa ni Kukosa UZALENDO katika nchi
“Mimi nimekuwa katika upinzani nimepigwa, nimewekwa ndani lakini siwezi nikaenda nje nikasema msipeleke msaada katika sekta ya elimu, afya huko ni kukosa uzalendo. Sikumtaja Zitto Kabwe ila kama alifanya hivyo ni kukosa uzalendo” Mwenyekiti CUF, Ibrahim Lipumba