Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 6:56 pm

PROF. LIPUMBA AWAUNGA MKONO MBOWE NA ZITTO KUDAI TUME HURU YA UCHAGUZI

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), nchini Tanzania Profesa Ibrahim Lipumba, amemuomba Rais wa nchi hiyo John Magufuli kukubali kukutana na viongozi mbalimbali wa vyama vya kisiasa nchini ili kujadili masuala mbalimbali likiwemo suala la Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Image result for PROF LIPUMBA

Lipumba ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Februari 10, katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam ambapo pia amemshauri kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ili kuviruhusu vyama kueneza sera zake kwa wananchi.

Image result for PROF LIPUMBA

“Sheria ya vyama vya siasa inataka kila chama kuwa na rejesta, lakini utekelezaji wa kipengele hicho unahitaji kuhamasisha wananchi.

“Kwa hiyo tunapohitaji mikutano ya hadhara si tu kueneza sera, pia tunataka kutekeleza mara kwa ya Sheria ya vyama vya siasa,” amesema Profesa Lipumba.

Amesema mchakato wa ukandamizaji demokrasia utafanikiwa ikiwa wananchi wakiwa wakiwamo wanachama wa chama hicho kutaja kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hata kama mazingira hayaruhusu kufanya hivyo.

Kuhusu CUF kusimamisha wagombea, amesema Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho limeshaamua kuwa litasimamisha wagombea katika ngazi zote Tanzania Baraza na Visiwani.

Aidha amelitaka Jeshi la Polisi kuielewa vema sheria ya vyama vya siasa na kuacha kuvizuia vyama vya upinzani kutekeleza haki yake ya kisheria ya kufanya mikutano.