Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:35 am

PROF. LIPUMBA AVITAKA VYOMBO VYA DOLA KUTOINGILIA MIKUTANO YA HADHARA

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema watafanya mikutano ya hadhara ya Kuhamasisha watu kujitokeza kwenye daftari la wapiga kura kwa kufuata taratibu huku akivitaka vyombo vya dola kutoingilia mikutano hiyo.

Image result for prof. ibrahim lipumba na waandishi wa habari

Kauli ya Prof Lipumba ameitoa leo Alhamisi Juni 27, 2019 wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ofisi za CUF Buguruni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasilisha maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi la CUF lililokutana hivi karibuni.

Profesa Lipumba amevitaka vyombo hivyo kutoingilia uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwaacha wananchi wapate haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.

“Tutafanya mikutano kwa kuwa hilo si kosa kisheria tunaomba polisi na vyombo vingine vya dola wasituzuie,” amesema Profesa Lipumba Amesema chama hicho kitafanya mikutano hiyo kwa nia njema ya kuisaidia Serikali ya Tanzania kuhamasisha watu wengi kujitokeza kujiandikisha.

Lipumba amesema Tume ya uchaguzi (NEC) haiana mvuto wa kuhamasisha watu, Hiyo kazi inafanywa vyema na vyama vya siasa kwa kuongea na wananchi umuhimu wa kujiandikisha.

“Hatuvunji sheria kwa kuwa hatutafanya kampeni mikutano yetu itakuwa ya amani na utulivu, tutakachotoa ni elimu na tutafanya kwa kufuata taratibu,” amesema Profesa Lipumba