- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
POLEPPLE: WALIOENGULIWA SEREKALI ZA MITAA NI KWASABABU YA UJINGA WAO
Dar es salaam: Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa wagombea walioenguliwa katika uchaguzi wa serikali za Mitaa ni kutokana na ujinga wao wa kutofuata sheria za uchaguzi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya Chama hicho, Katibu wa Itakadi na Uenezi Hamphrey Polepole amesema kuwa CCM haihusiki kwa kuenguliwa kwa wagombea katika uchaguzi wa serikali za Mtaa kwani wao ndio wamekosea kutofuata sheria.
Amesema kuwa CCM iliwekeza katika elimu kuhusiana na uchaguzi wakati vyama vingine vilishindwa kufanya hivyo badala yake wanaitupia lawama kuwa CCM imefanya hujuma.
Polepole amesema kuwa walijipanga katika uchaguzi huo na watashinda kwa kushindo kutokana na kazi walizozifanya za utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2015.
Amesema kuwa CCM ni Chama kikubwa hakiwezi kushindana vyama ambavyo hata taratibu za uchaguzi .Aidha ameema kuwa na watu wengine walikuwa wanagombea katika vyama visivyokuwa katika orodha ya msajili.
Polepole amesema serikali kteuacha kuwaonea huruma kwani wanashindwa kufuata taratibu na mwisho wa siku wanategemea.
Amesema kuwa vyama visitafute huruma wakati vinashindwa kuwekeza elimu kwa wanachama wao. Polepole anasema kuwa watu wengine wameenguliwa kwa kutokuwa na kazi wakihojiwa kazi wanazozifanya wanasema tupo tunapambana hapo.