Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 8:01 pm

POLEPOLE : VYAMA VYA UPINZANI VIMEKOSA UHALALI WA KUDAI MAREIDHIANO

Kilimanjaro: Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Tawala cha Tanzania CCM, Humphrey Polepole amesema vyama vya upinzani nchini vimekosa uhalali wa kudai maridhiano ya kitaifa kwa sababu vimeshindwa kuzingatia hatua za msingi na awali kabla ya kufikia hatua ya maridhiano ambayo wao wanayatakata.

Polepole ametoa kauli hiyo katika muendelezo wa maadhimisho ya miaka 43 ya Chama CCM katka wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro yaliyobeba kauli mbiu ya ‘Tuliahidi, Tumetekeleza na tunaahidi tena kuchapa kazi kwa juhudi, ubunifu na maarifa zaidi’.

Vyama vya upinzani hasa Chadema, ACT-Wazalendo na NCCR-Mageuzi siku za hivi karibuni vimekuwa vikipiga kelele vikitaka meza ya mazungumzo ili mambo mbalimbali ya kitaifa yanayolalamikiwa yatatuliwe.

Polepole amesema amekuwa akifuatilia mijadala na mapendekezo yaliyotolewa na vyama vya upinzani kuhusu maridhiano.

“Maridhiano ni hatua na vyama vya upinzani nchini vimeshindwa tangu mwanzo kuzingatia hatua za msingi na za awali, na hata sasa kabla ya kufikia hatua ya maridhiano.” “Hilo linawakosesha uhalali wa kutaka maridhiano, kwa sababu maridhiano huanza kwa kuwa na uelewa wa pamoja katika mambo ya msingi, pili kujenga muafaka na tatu kuwa na maridhiano yenyewe,” alisema Polepole

Akifafanua kuhusu dhana na nadharia ya maridhiano, Polepole amesema kuwepo kwa uelewa wa pamoja kujua Watanzania wanataka nini, kazi kubwa ya maendeleo ambayo imekwisha kufanyika nchini na kubadilisha kabisa hali na ustawi wa watu.

“Muafaka wa kitaifa kwa maana ya kukubaliana katika kazi nzuri ambayo imefanyika na katika yale ambayo hakuna muafaka ndio tunakwenda katika maridhiano,” amesema. Polepole alitumia nafasi hiyo pia kuelezea ni namna gani CCM kimejipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 huku akiangazia mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka 43