- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
PICHA: NIMEKUSOGEZEA MATUKIO YOTE YA UTOAJI TUZO ZA TFF
Dar es salaam: Shirikisho la soka Tanzania TFF Jana limehitimisha msimu wa ligi kuu ya Tanzania bara maarufu kama VPL kwa kuwakabidhi Tuzo wachezaji waliofanya vizuri katika ligi hiyo. Hafla hiyo iliyo hudhuriwa na viongozi wa TFF na Viongozi wengine kutoka serekalini na wasanii mbalimbali(skylight band)
HAYA NDO MATUKIO
Hapa timu ya Yanga Africa ikikabidhiwa Tuzo ya mshindi wa kwanza
Tuzo ya mshindi wa pili imekwenda kwa Simba ambao hawakushiriki Hafla hiyo
Timu yenye nidhamu imekwenda kwa Mwadui FC
Mwamuzi bora wa mwaka ni El sasi wa Dar es salaam
Manaula wa Azam ameshinda tuzo ya kipa bora
Mchezaji bora wa kigeni ilikwenda kwa Niyonzima kutoka Yanga
Mchezaji bora chipukizi inakwenda kwa Mbaraka Abeid wa kagera sugar
Tunzo ya kumuenzi mchezaji wa mbao aliye fariki inachukuliwa na shabani kutoka Azam
Goli bora la mwaka anachukua Kichuya wa simba fc
HII NDIO LIST YA TUZO ZOTE
- Azam FC- Wachukua tuzo ya timu iliyoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu VPL na wameshinda shilingi milion 24
- Kagera Sugar- Wachukua tuzo ya timu iliyoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu VPL na wameshinda shilingi milion 30
- Simba SC- Wachukua tuzo ya timu iliyoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu VPL na wameshinda shilingi milion 44
- Yanga FC- Wachukua tuzo ya timu iliyoshika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu VPL na wameshinda shilingi milion 84
- Mfungaji Bora-Msuva na Abraham Mussa na wameshinda shilingi Milion 5 na laki 8 kila mmoja
- Timu yenye Nidhamu- Timu yenye nidhamu wameshinda Mwadui FC na wameshinda milion 17 na laki 5
- Mwamuzi bora wa mwaka- Mwamuzi bora wa mwaka ni Eli Sasi wa Dar es salaam
- Kocha bora- kocha bora wa mwaka ni Mecky Mexime kutoka Kagera na ameshinda shilingi milion 8
- Kipa Bora- Kipa bora wa mwaka ni Manula wa Azam FC na ameshinda mil 5 laki 8
- Mchezaji Bora wa Kigeni- Mchezaji bora wa kigeni ni Niyonzima kutoka Yanga FC na ameshinda mil 5 na laki 8
- Mchezaji Bora Chipukizi- Mchezaji bora Chipukizi ni Mbaraka Abeid kutoka Kagera Sugar na amejishindia mil 4
- Tuzo ya Ismail , Tuzo ya kumuenzi Mchezaji wa Mbao FC Ismail aliyefariki uwanjani inachukuliwa na Shaban kutoka Azam
- Goli Bora la mwaka- Tuzo ya Goli bora la mwaka Ligi kuu Tanzania Bara anachukua Kichuya kutoa Simba SC na ameshinda mil 3
- Mchezaji Bora wa Mwaka-Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Ligi Kuu Tanzania Bara ni Mohamed Hussen kutoka Simba