- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
(PICHA +8): KILICHOTOKEA BAADA YA KIPA WA CHELSEA KUGOMA KUTOKA UWANJANI
Kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga Jana usiku aligomea uwamuzi wa meneja Maurizio Sarri wa kutaka kumbadilisha uwanjani katika dakika za lala salama katika mechi ya fainali ya kombe la Carabao, kitendo ambacho kilimfanya meneja huyo abaki na hasira kubwa nje ya uwanja huo hata kimuonekano huku akipiga teke guo za wachezaji na machupa ya maji.
Kabla ya kutaka kutolewa Arrizabalaga alipata majeraha ya kubanwa kwa maumivu ya msuli, na wakati huo mechi ikiwa 0-0, Sarri alikuwa anajitayarisha kumuingiza kipa wa akiba Willy Caballero katika nafasi ya Kepa kabla ya awamu ya mikwaju ya penalti.
Sasa kilichotokea baada ya hapo, Kipa huyo na Meneja wake walinyoosheana vidole kwa muda kadhaa na kupiga kelele kiala mmoja, lakini baada ya kipa huyo kogoma katu kuondoka uwanjani Meneja wake Sarri ilimlazimu asalimu amri na kumuoacha kipa huyo kuendelea kudaka.
Refa Jonathan Moss alikimbia kumfuata Sarri kuthibitisha iwapo kweli anataka Arrizabalaga aondoke au la, na Sarri, ilibidi abadili msimamo wake kabla ya kuondoka kwa hasira , na muda mfupi baadaye kurudi, akimuacha kipa wa akiba Caballero akiwa amesimama amesha jitayarisha kwa kuingia.
Arrizabalaga alifanikiwa kuokoa mkwaju wa Leroy Sane - lakini Raheem Sterling alifunga bao la ushindi katika mikwaju hiyo ya penalti wakati Manchester City walipotuzwa mabingwa wa taji hilo la Carabaokwamwaka wa pili kutokana na ushindi wa mwisho wa mabao 4-3.
Sarri hakuonekana kuonyesha hisia zozote, wakati wachezaji wake wakionekena kuhuzunishwa kwa kushindwa.