Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:23 am

PAUL MAKONDA "NDOA ZOTE ZA DAR ES SALAAM KUSAJILIWA

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda amesema kuna mpango wa kuanzisha kanzidata yaani mfumo wa kusajili ndoa zote zilizopo kwenye mkoa wake ili kupunguza utapeli na ujanja ujanja wanaofanyiwa wanawake kwa kudanganywa kuolewa.

“Tutaanza kuangalia na kupata uzoefu kwa wenzetu wa SADC ambao kama haya wanashughulikiaje na mkutano ukiisha tutajadiliana kama mkoa tunawezeshaje usajili huo,” amesema

Kanzidata hiyo itahusisha usajili wa ndoa zote ili wanaume waliooa waweze kubainika na kuwanusuru wanawake wasitapeliwe na kuumizwa mioyo kwa kutegemea ndoa.

Makonda amesema pamoja na kanzidata hiyo atatumia mkutano wa SADC kupata uzoefu kutoka kwa nchi nyingine kufahamu namna gani wanakabiliana na utapeli wa aina hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa amesema kumekuwepo na malalamiko mengi ya wanawake kuumizwa hivyo wakati umefika wa kuanza kushughulikia.

“Kanzidata hii itawasaidia wanawake wasitapeliwe, mtu akitaka kukuoa utaenda mtandaoni na kuangalia taarifa zake, utabaini kama ameoa au la na vilevile itawasaidia hata wanawake ambao wameolewa ili kuzuia waume zao wasioe kwa siri,” ameongeza