Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:27 am

NICHE NEWS : SERIKALI YAIPONGEZA MUHIMBULI

Serikali imepongeza juhudi zinazofanywa na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuboresha huduma na kuwawezesha watalaam kusoma ili wapate ujuzi zaidi na kutoa huduma bora na za kibingwa.

Kauli hiyo imetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulusubisya wakati akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo kupitia Idara ya Usingizi.

“Naona mabadiliko makubwa hapa Muhimbili, mmeongeza vyumba vya upasuaji, Vyumba vya wagonjwa mahutuni (ICU) na pia mnaendelea kuboresha huduma zingine kwakweli hatua hii ni ya kupongezwa na ninaomba muendelee kujituma kwani hospitali hii inategemewa kwa sababu mna watalaam wengi waliobobea hapa,’’ amesema Dk. Mpoki.

Kuhusu kusomesha wataalam, Katibu Mkuu amesema hatua hiyo ni nzuri kwani watalaam hao watapata fursa ya kuwatawafundisha wengine ili nao wapate ujuzi .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema MNH inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa wataalam katika Idara ya Usingizi na kwamba hospitali inaendelea kutatua changamoto hizo.