- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:WATANZANIA WATOLEWA HOFU JUU YA USALAMA WA AFYA ZAO
DODOMA: SERIKALI imesema kuwa usalama waAfya za watanzania upo salama mikononi mwa Mamlaka ya Chakula na dawa nchini (TFDA)kutokana na umakini na uadilifu walionao katika ukaguzi wa vyakula na dawa.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,wazee,jinsia na watoto,DK.HAMISI KIGWANGALA wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Temeke,ABDALLAH MTOLEA.
Mbunge huyo,alitaka kujua TFDA inafanya jitihada gani kuhakikisha chakula ghafi kinakuwa salama kutokana na kuwepo kwa tabia ya baadhi ya wauzaji na wazalishaji kuuza bidhaaa zilizoisha muda wake kwa hasara katika mahoteli na Migahawa na hivyo kuwepo kwa sumu ya vyakula (food poison).
Dk.KIGWANGALA amesema kuwa malighafi ambazo zinatengeneza vyakula ni salama kutokana na umakini mkubwa na uadilifu unaofanywa na TFDA hivyo kama ikitokea kunakuwepo nasumu katika vyakulainakuwa imetokana na maandalizi hafifu ya waandaaji wa vyakula.
Hata hivyo amefafanua kuwa kutokana na kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa Maabara za TFDA, hivi sasa wanaongeza uwezo wa kujenga maabara mpya katika kila kanda ili kutanua wigo wa kuwafikia wananchi katika kuwahudumia.