- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:WANAFUNZI 3000 KIDATO CHA NNE WALIOFAULU WAMEACHWA
DODOMA: JUMLA ya Wanafunzi 93,018 waliomaliza kidato cha nne mwaka jana, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na Vyuo vya ufundi mwaka huu huku wanafunzi 3000 wameachwa.
Wanafunzi hao waliochaguliwa ni wale wenye ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu.
Hayo yameelezwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,GEORGE SIMBACHAWENE wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Waziri SIMBACHAWENE amesema kuwa wanafunzi hao waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka huu,wanatoka kwenye Shule za Serikali na binafsi zipatazo 351 zikiwemo shule 17 mpya ambazo zimepangiwa wanafunzi.
Hata hivyo amebainisha kuwa muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka 2017 utaanza Julai 17 na wasipo ripoti nafasi zao watapewa watu wengine na wale wakidato cha sita masomo yataanza julai 3 mwaka huu.