- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:WAANDISHI WA HABARI ZA BUNGE WAPIGWA MSASA
DODOMA: WAANDISHI wanaoripoti habari za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametakiwa kuandika habari zenye maslahi kwa jamii na kuacha kushabikia habari za ukiukwaji wa kanuni unaofanyika katika vikao vya Bunge.
Hata hivyo Wamewataka waandishi wa habari kuhakikisha kuwa wanapata Taarifa kamili na kutembea katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ili kuweza kufahamu sheria mbalimbali pamoja na mipaka yake.
Naye Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini, Deodatus Balile akizungumza wakati wa kutoa mada amewataka waandishi hao kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na Bunge ili waweze kufanya kazi yao ya kuhabarisha umma kwa Uhuru kuliko kukinzana na kanuni za Bunge.
Naye mmoja wa washiriki wa semina hiyo Joyce Kasiki ambaye ni mwandishi wa habari wa gezeti la Jambo Leo amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidi kuongeza weledi katika kuandika habari za bungeni.
Amesema kuwa semina kama hizo zinatakiwa kutolewa mara kwa mara kwa maandishi kwani waandishi hao wamekuwa wakibadilishwa kila wakati kushiriki katika vikao vya bunge,hivyo itasaidi hata kwa wale ambao ni mara ya kwanza kuanza kuingia bungeni.