Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:45 am

NEWS:U-DOM ''MEI MOSI IWE NA TIJA KWA WAFANYAKAZI''

Dodoma: WAADHILI wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wametaka maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi nchini yalenge kuboresha masilahi ya wafanyakazi.

Wakizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa Elimu ya juu (THTU) Nashon Maisori,amesema maadhimisho hayo yalenge kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Kiongozi huyo ameleza kuwa wao kama watumishi wa Chuo kikukuu cha Dodoma waliamua kufanya maadhimisho yao katika ukumbi wa umoja wa vijana kwa lengo la kubadilishana mawazo na kuona ni jinsi gani ya kuweza kuweka mikakati ya utendaji wa kazi zao.

“Sisi tumeamua kukusanyaka hapa kwa lengo la kufurahi pamoja hii sikukuu ya wafanyakazi lengo lake ni kukaa na kutathimini kazi ambazo wanatakiwa kuzifanya sambamba na kuweka mikakati ya kutaka kuboreshewa maslahi yao ili kazi iweze kuwa na ufanisi.

“Hatukuona sababu yoyote ya kufanya maandamano wala kutengeneza mabango lakini tumeamua kukutana pamoja ili tuweze kula na kunywa pamoja na kujadiliana ni jinsi gani ya kuboresha kazi zetu huku tukiangalia ni jinsi gani ya masilahi yetu yatakuwa yameboreshwa” amesema Maisori.

Naye katibu wa THUTU Udom Gerald Shija amesema maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi yasitumiwe kisiasa badala yake yalenge zaidi mahitaji ya siku husika.

Alisema siku kama hiyo ni muhimu kwa wafanyakazi kwani wafanyakazi wengi wanakuwa na matumaini ya kusikiliza nini kinaboreshwa.

“Mara nyingi siku kama hiyo ni siku ya matumaini kwa wafanyakazi kwani utarajia kupandishwa mishahara,kupandishwa vyeo pamoja na kupata matumaini mbalimbali katika kazi zao.

“Siku ya maadhimisho ni siku pekee ambazo wafanyakazi utegemea kulipwa malimbikizo yao kwani mahudhui ya siku hiyo ni kudai au kutetea haki zao ambazo wakati mwingine uchelewa au uelekea kupotea” alieleza Shija.

Naye mhadhili wa Chuo Kikuu cha Udoma na mwenyekiti wa wanataaluma wa elimu ya juu Poul Loisulie, alisema sikukuu ya wananyakazi ni muhimu sana kwa wafanyakazi kwani ni siku yao ya kuwasilisha kilio chao kwa viongozi wa serikali ambao nidio waajiri.

Amesema waajiri wanatakiwa kutambua kuwa siku hiyo ndiyo siku ya kutatua kero za wafanyakazi ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu.