Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 1:44 pm

NEWS:TRA YAVIFUNGIA VITUO 15 VYA MAFUTA DOM

DODOMA: Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Dodoma imevifungia vituo 15 vya kuuzia mafuta vilivyopo katika Wilaya ya Dodoma kutokana nakutokuwa na mashine za kutolea risiti zilizofungwa moja kwa moja kwenye pampu za kutolea mafuta.

Akizungumza na wauzaji wa mafuta kwenye vituo vilivyofungwa, Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Thomas Masese amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na lipo kwa mujibu wa sheria kwa kuwa wamiliki wa vituo hivyo vya mafuta walipewa muda wa kutosha kufunga mashine hizo lakini hata hivyo wamekaidi maagizo ya serikali.


Naye Mwenyekiti wa Chama cha waendesha vituo vya mafuta Tanzania (TAPSOA) Kanda ya Kati, Faustine Mwakalinga amesema kuwa zoezi hilo la kuvifungia vituo vya mafuta linaweza kuleta madhara makubwa kwa ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuwa vituo vingi vya mafuta hasa vilivyoko Wilayani havijafungwa mashine hizo.



Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme ambaye ameongoza zoezi hilo amesema kuwa vituo hivyo vimefungwa kutokana na kuendesha biashara kinyume na sheria na kutoa wito kwa wafanyabiashara wote wa Wilaya ya Dodoma kufunga mashine hizo ili serikali iweze kupata mapato yake yanayotokana na kodi kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wake.


Vituo vilivyofungwa mpaka sasa ni TIOT kinachomilikiwa na Ahamed Shabiby, Ibra General Interprises, TSN, Oil Com (vituo 3), Camel (Oilvituo 2), Lake Oil (vituo 2), State Oil, GP 88 (vituo 2), Afroil.