- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:TAKUKURU DOM YAKOA ZAIDI YA MILIONI 135.
DODOMA: Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa[TAKUKURU] Mkoa wa Dodoma imeokoa Jumla ya Tsh.Milioni 135,laki 9 ,48 elfu na mia 193 kwa kipindi cha miezi 6.
Hayo yameelezwa leo na Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Dodoma Sosthenes Kibwengo amesema Fedha hizo zimeokolewa kwa kipindi cha Miezi 6 kuanzia Mwezi Januari,hadi Juni ,2019.
Kibwengo amesema kwa kipindi cha miezi sita pia zimedhibibitiwa Jumla ya Tsh.Milioni 322,laki 3 ,48 elfu na mia 989.
Hata hivyo ameendelea kwa kubainisha kuwa katika kipindi hicho cha miezi 6 kuanzia Januari hadi Juni ,2019 TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imepokea jumla ya Malalamiko 231 ya vitendo vya rushwa .
Kibwengo amesema asilimia 28% ya Malalamiko hayo yanatoka Serikali za mitaa [TAMISEMI],Ardhi kwa asilimia 26.5%,Polisi 7% na mahakama malalamiko kwa asilimia 6% na asilimia zilizobaki ni kwa sekta nyingine huku akitaja Wilaya iliyo na Malalamiko mengi ni Wilaya ya Dodoma Mjini.
Pia amesema kuanzia mwezi huu wa Agosti ,2019 wanatarajia kufungua ofisi za TAKUKURU Eneo la Chemba huku akitoa wito kwa wananchi kuwa na ushirikiano na Taasisi hiyo na kuweza kuitumia namba ya bure 113 pindi wanapoona vitendo vya rushwa.