Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:46 pm

NEWS:NCHEMBA AVIWAKIA VYAMA VYA SIASA

DODOMA: WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi,MWIGULU NCHEMBA amevitaka Vyama vyote vya siasa nchini kufuata taratibu pale vinapotaka kufanya mikutano ya hadhara.

Waziri NCHEMBA ametoa kauli hiyo leo,Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Iringa Mjini PETER MSIGWA.

Mbunge huyo alitaka kujua kauli ya Serikali kama demokrasia inafuatwa kutokana na Polisi kufanya upendeleo katika utoaji vibali hasa kwaWanafunzi wa CHASO wa chama cha Chadema wanazuiliwa kufanya mahafali.

Mwigulu Nchemba amesema duniani kote Vyama vinafuata taratibu hivyo wasifanye vitu kimazoea hivyo chama chochote kifuate taratibu kinapotaka kufanya mikutano.

Hata hivyo amesema taratibu ziko wazi na kwamba Jeshi halifanyi wala upendeleo katika utoaji wa vibali.