- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:MWANAMKE AUAWA KIKATILI NA MUMEWE AKIDAI KUHONGA KODI YA MAJENGO
RUKWA: WATU wawili wamekufa katika matukio tofauti katika mkoa wa Rukwa, akiwemo mkazi wa Kijiji cha Mafulala Manispaa ya Sumbawanga, Anna Kashamsakula (35) aliyeuawa kikatili baada ya kuchinjwa na mumewe, baada ya kumtuhumu kumhonga mwanamke mwingine Sh 30,000.
Mshtakiwa alipewa fedha hizo na mkewe ili akalipe kodi ya jengo, waliyokuwa wakidaiwa na Mamlala ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Rukwa. Akithibitisha, Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema kuwa mauaji hayo yalitokea Julai 27, mwaka huu saa sita usiku katika kijiji chaMafulala.
Akifafanua, alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi, ambapo marehemu alimpatia mumewe Sh 30,000 ili akalipie kodi ya jengo, ambapo hakulipa bali alienda kutumia na mwanamke mwingine.
Inadaiwa kuwa mume huyo alipewa kiasi hicho cha fedha na mkewe Julai 25, mwaka huu, lakini hakurudi hadi siku iliyofuata, ambapo ugomvi wa maneno uliibuka miongoni mwao hadi Julai 27, mwaka huu mume huyo alipoamua kumuua mkewe na kutokomea kusikojulikana.