- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:MKAPA MGENI RASM JUBILEI YA MIAKA 100 YA UPADRI
DODOMA: RAIS wa awamu ya Tatu Benjamini Mkapa kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha Jubilei ya miaka 100 ya Upadri yatakayoshirikisha zaidi ya mapadri na maaskofu 520.
Ibada hiyo itaongozwa na Rais wa Mashirika ya Kipapa kutokana nchini Vatican, Mhashamu Askofu Protas Rugambwa akimwakilisha papa Benedict 16.
Ibada hiyo itakayofanyika katika Kituo cha Hija kilichopo eneo la Mbwanga kata ya Miyuji mjini hapa imetanguliwa na Ibada ya Ufunguzi iliyofanyika katika kanisa kuu la Romani Katholiki Paul wa Msalaba jimbo kuu la Dodoma.
Katika ibada hiyo, Askofu Kiongozi wa Jimbo Katholiki kigoma, Joseph Mlola, amewaasa waumini wa kanisa katoliki kote nchini kutokuwa chachu ya kuwashusha Mapadri na Maaskofu kiimani na badala yake watumie muda mwingi kuwaombea ili waendelee kusimama katika maadili ya na kuuishi utume wao.
Mbali na hayo amesema, wakati mwingine waaumini badala ya kutekeleza wajibu wao wa kuwaombea viongozi wao wa kidini wamekuwa chanzo cha kusababisha viongozi hao kuingia katika mambo ambayo yanakwenda kinyume na utume wao.
Pia amewataka kutumia mapadri kutumia maadhimisho hayo kutafakari kama wanakwenda sawa na nadhiri walizoziweka wakati wakipokea madaraja ya utume huo.
“Waumini pamoja na viongozi wa dini tumieni maadhimisho haya kudumisha uopendo, amani mshikamo, ikiwa ni pamoja na kujua gharama ya upendo kwa jamii inayowazunguka kwa kuwasaidia wenye shida na wahitaji,”amesisiza.
Kwa upande wake, Askofu wa Jimbo Katoliki Jimbo la Mwanza Askofu Yuda Thadeus Ruwaichi, ametoa wito kwa mapadri wanaotarajia kupokea madaraja ya upadri, akiwataka kutambua kuwa wito ni zawadi kutoka kwa Mungu na si kitu ambacho wanadamu wanacho.
Amesema wakati wanatarajia kuingia katika nadhiri hiyo, wanapaswa kutafakari, kijipima, kujilea na kulelewa kwa mambo ya ukristo na si ya kibinadamu.
“Mkifuata ukristo na matendo yake, mtaingia katika daraja hilo kama mtu anayejitoa sadaka kwa ajili yaw engine na si vinginevyo,”amesema.
Kuhusu maadhimisho hayo alisema, ni tukio la kihistoria ambalo linawapa fulsa ya kutafakari na kumshukuru Mungu na kuendelea kuomba kusudi waendelee kupata mito ya vijana wenye imani waadilifu, wacha Mungu, wakarimu ambao wako tayari kujitoa kwa kristo watumikie katika kanisa lake.
Askofu Rwaicha nikipindi pia cha kijitathimini katika yale waliofanya vizuri kama wenye daraja la upadri, wajiimarishe na kule ambapo hawakufanya vizuri wajipange weweze kufanya kwa mtindo ambao unalijenga kanisa na kumtukuza Mungu.
Mwasham Rwaichi, amebainisha kuwa hali ya mito inatofautiana, kuna majimbo yanahangaika na yapo yanafanya vyema na sababu za tofauti hizo hazijafanyiwa kazi kiasi cha kutosha.
“Kuna haja ya kuzitafakari changamoto hizo na kurudi kupiga magoti mana wito ni zawadi kutoka kwa Mungu, kule ambapo kuna mito mizuri wamshukuru Mungu na ambapo kunachangamoto wazidi kupiga magoti kumuomba Mungu,”amesema.