- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:MGOMO WA DALADALA WAITIKISA DODOMA.
DODOMA: Madereva Daladala katika kituo cha magari cha Sabasaba Jijini Dodoma wamegoma kufanya safari wakishinikiza wamachinga kuondolewa kutokana na ufinyo wa nafasi katika eneo hilo.
Mgomo huo uliyoanza tangu majira ya asubuhi umesababisha umati mkubwa wa watu kushindwa kuendelea na majukumu yao huku wengine wakilalamika biashara zao kudoda.
Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya madereva wamesema kuwa,wamegoma kutokana na wamachinga kutokuwa na utaratibu mzuri wa kufanaya biashara.
Hata hivyo,baadhi ya abiria waliokuwa wakifanaya safari zao za kutoka na kuingia ndani ya stand hiyo wanaeleza athari za mgomo huo, Franco James unasababisha watu kushindwa kufika katika maeneo yao ya kazi.
Akizungumza na madereva hao mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi mbali na kuomba madereva hao kuendelea kusafirisha, amepiga marufuku baadhi ya biashara ikiwemo uchomaji mshikaki .
Mgomo huo sasa umekwisha na shughuli zimerudi kama kawaida katika kituo cha daladala cha sabasaba Jijini hapa.