Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 4:26 pm

NEWS:MBUNGE DITOPILE, ILANI NDIO SILAHA KUBWA TUITEKELEZE.

DODOMA: Mbunge wa viti maalum Mariam Ditopile mei 8 ameshiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Ibugule wilayani Bahi mkoani Dodoma.


Kikao hicho kilikuwa na lengo la kupokea uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kuanzia mwaka 2016 hadi april 2019.


Akiwasilisha taarifa hiyo diwani wa Kata ya Ibugule Blandina Magawa ametaja mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho ikiwemo ujenzi wa shule,maabara,vituo vya afya,umeme ,utawala bora, ulinzi na usalama na kutatua migogoro ya mipaka.


"Pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto tunazopambana nazo ikiwemo akina mama kujifungulia nyumbani,mwitikio mdogo wa wazazi kuchangia chakula mashuleni na suala la utoro na mimba mashuleni,"alisema diwani huyo.


Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo mbunge Ditopile pamoja na mambo mengine amehimiza utekelezaji wa Ilani kwa kuwa ndio silaha kubwa katika kuelekea chaguzi za serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020.

"Tumeona Sh bilioni 1.5 zimeletwa Bahi kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya, umeme umefika vijijini uwongo kweli?watoto wetu wanasoma shule bure hii yote ni kazi ya serikali yetu chini ya Rais wetu, jembe letu Dokta John Pombe Magufuli, hivyo tusiwatupe viongozi wetu, tuwaunge mkono na tuendelee kuwapa moyo kwa kuwa pembeni yao, "alisisitiza mbunge huyo.


Ameipongeza kata hiyo kwa kufanya vikao vilivyotoa fursa kwa wajumbe kuuliza maswali na kujibiwa ikiwa ni namna ya kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kukomaza demokrasia mashinani aliouzindua Katibu Mkuu wa CCM dokta Bashiru Ally.


Katika kikao hicho mh Ditopile ametoa bendera za CCM kwa ajili ya mashina na matawi yaliyopo katika kata hiyo.