Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 5:13 pm

NEWS:MBUNGE AHOJI KUZAGAA KWA DAWA FEKI ZA KILIMO NA MIFUGO

DODOMA: SERIKALI imekiri kuwepo changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uingizwaji wa Dawa za mifugo na kilimo ambazo hazikidhi viwango.

Mbali na kuwepo kwa changamoto hiyo ya kuingizwa madawa ya mifugo na mazao yasiyo kidhi kiwango serikali imefanikiwa kukamata lita 14,600 za viatirifu kwa mwaka huu ambazo zilikamatwa kwa kuingizwa nchini kwa njia ya panya.

Hayo yameelezwa leo bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,William Ole Nasha,alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum,Sikudhani Chikambo (CCM).

Katika swali la nyongeza la mbunge huyo alitaka kujua serikali imejipangaje katika kukabiliana na uingizwaji wa dawa za mifugo na kilimo ambazo hazikidhi kiwango kinachotakiwa.

Pia amelitaka kujua ni kwanini dawa hizo zimekuwa zikipatikana hapa nchi na kuwafikia wakulima na wafugaji jambo ambalo linawasababishia wafugaji na wakulima hao kushindwa kufikia Marengo ambayo wanakuwa wameyakusudia.

Naye mbunge wa Msalala,Ezekiel Maige (CCM)katika swali la nyongeza alitaka kujua serikali inatoa tamko gani kwa bodi ya Pamba ambayo ilikuwa ikisambaza dawa ya pamba ambayo ilikuwa ikiitwa ninja lakini haikuweza kuua wadudu na kusabaisha wakulima wengi wa pamba kupata hasara

.

Awali katika swali la msingi la mbunge Sikudhani Chikambo (CCM) alitaka kujua serikali inajipangaje katika kuhakiki dawa za kilimo kabla haizijaanza kutumika.

Pia alitaka kujua serikali imejipangaje katika kuthibiti bei ya dawa za mifugo pamoja na dawa za kilimo ambazo hazikithi kiwango.

“Kumekuwa na tatizo la ungizwaji wa dawa za kilimo na mifugo ndani ya nchi zisizokidhi vigezo na bei ya dawa hizo zinaongezeka siku hadi siku na kufanya wakulima na wafugaji wadogo kukosa maendeleo.

“Je serikali inachukua hatua gani za kuhakikisha dawa hizo kabla hazijaingia nchini,je serikali ina utaratibu gani wa kuthibiti bei hizo” amehoji.

Akijibu maswali hayo ya Nyongeza Ole Nasha alisema serikali imekuwa ikipambana na uingizwaji wa dawa ambazo hazikithi viwango.

Kuhusu suala la dawa ya pamba ambayo ilifahamika kwa jina la Ninja,alisema kwa sasa hivi uchunguzi unaendelea ili kubaini tatizo la dawa hiyo kutoua wadudu inatokana na nini kwani bado kuna mvitano kati ya wakulima, matumizi ya dawa yenyewe pamoja na ubora wa dawa.

Akijibu swali la msingi Ole-Nasha alisema Ukaguzi wa kufuatilia dawa katika soko hufanyika ili kuhakikisha kuwa dawa zilizopo katika soko zinaendelea kuwa na ubora uleule kama wakati ziliposajiliwa.