- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:MAMLAKA YA ELIMU NCHINI TEA KUFANYIA UKARABATI SHULE KONGWE 88
DODOMA: MAMLAKA ya Elimu nchini (TEA)imesema inatarajia kukarabati Shulekongwe za sekondari nchini takribani 88 ambazo majengo yake yapo katika hali mbaya,lengo ikiwa ni kutoa hamasa ya usomaji kwa Wanafunzi.
Hayo yalielezwa jana mjini hapa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo nchini,Graciana Shirima wakati wa makabidhiano ya ukarabati wa Shule ya Sekondari Msalato kwa MkandarasiLucas Ngowo wa Kampuni ya consultationlimited ambapo utasimamiwa na Shrika la Numba la Taifa la Mkoani hapa(NHC).
Bi.Shirima alisema kuwa Mamlaka hiyo imeamua kufanya ukarabati huo wa shule hizo kongwe kutokana na majengo yake kuchakaa kwa ni ni ya muda mrefu ambapo hadi sasa jumla ya shule 10 tayari zimeshakarabatiwa na kukabidhiwa.
Alizitaja Shule hizo ni pamoja na Ilboru Sekondari,Suma JKT,Same Sekondari,Mzumbe Sekondari,Kilakala sekondari,MwengeSekondari,Pugu sekondari,Tabora boys na Tabora girls.
“Ukarabati katika Shule ya Msalato utakuwa wa awamu nne ambapoutafanyika ukarabati wa majengo ya mabweni ikiwemo mifumo ya maji na umeme, na utagharimu kiasi chaMilioni 939.187 kwa mujibu wa mtaalam mshauri,”alisema
Aidha alibainisha kuwakatika Mkoa wa Dodoma, shule nyingine ambazo zitafantiwa ukarabati ni pamoja na Dodoma Sekondari,Bihawana Sekondari ikiwemo Kondoa girls.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msalato Sekondari,Line Chanafi alimshukuru Rais John Magufuli kwa kuwema mfumo wa elimu bure pia aliishukuru Mamlaka hiyo ya elimu nchini TEA,kwakufanya ukarabati wa shule yao.
Bi. Chanafi alisema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo ya shule hasa mabweni pia vyumba vidogo vya madarasa ambavyo havikidhi mahitaji ya wanafunzi hivyo wanahitaji madarasa mengine.
Kwa upande wake Meneja wa Shrika la Nyumba la Taifa,mkoani Dodoma,Joshua John amesema watatekeleza mradi huo wa ukarabati kwa uadilifu ikiwa ni pamoja na kuzingatia muda na kwa maslahi ya Taifa.
“Hii ni heshima kubwa kwetu kama Shrika la nyumba hatutaiangusha Mamlaka ya elimu bali tutafanya kazi vizuri na kwa muda uliopangwa,”alisema.
Naye Mshauri elekezi ambaye atafanya ukarabati wa shule ya Mslato ,Lucas Ngowo wa qD consultation LTD,alisema kuwa walifanya tahtmini lakini changamoto ipo katika miundombinu ya maji taka na umeme licha ya kuwepo kwa ubovu wa majengo na kuahidi kutekeleza kazi hiyo.
“Tutatekeleza kazi hii ipasavyo kwakuzingatia muda,ubora wa majengo na thamani ya pesa ambayo haitazidi kiwango hicho cha pesa zilizopangwa kutukeleza kazi hiyo,”alisema.