- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:LOWASSA-TUNDU LISSU ANAENDELEA VIZURI
Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Edward Lowassa leo Septemba 11, 2017 amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu hospitali mjini Nairobi Kenya baada ya mbunge huyo kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017.
Edward Lowassa ambaye leo ameungana na baadhi ya watu wengine kwenda kumjulia hali kiongozi huyo amesema mbunge huyo sasa anaendelea vizuri na anaendelea na matibabu hata hivyo kiongozi huyo amesema kitendo alichofanyiwa Tundu Lissu ni kitendo cha kusikitisha kwa Tanzania.
"Mapema leo nilipomtembelea Mbunge, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na rafiki wa karibu Tundu Lissu, anaendelea vizuri kiafya, ila hizi ni nyakati za kusikitisha kwa Tanzania, kila mmoja kwa nafasi yake tuendelee kumuombea aweze kupona kabisaa" alisema Edward Lowassa
Mbunge Tundu Lissu yupo nchini Kenye akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi tano na watu wasiojulikana akiwa Makao Makuu ya Tanzania Dodoma.