- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:KESI YA KUPINGA KUTENGULIWA KWA CAG PROF. ASSAD IMEANZA LEO KUSIKILIZWA
Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania masjala Kuu Dar es Salaam hatimaye imeanza kusikiliza kesi ya kikatiba (usikilizwaji wa awali) iliyofunguliwa na Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Zuberi Kabwe kuhusu utenguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Asaad na Rais Kumteua Mrithi wake Charles Kichere.
Kesi hiyo imeanza kutajwa leo Jumanne Januari 28, 2020 katika mahakama Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuangalia taratibu za awali za mwenendo wa kesi hiyo ambazo ni pamoja na pande husika kukabidhiana nyaraka zinazohusu kesi hiyo, kabla ya kuendelea na hatua nyingine.
Zitto ambaye pia ni kiongozi wa chama hicho amefungua kesi hiyo dhidi ya Rais wa Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Charles Kichele na CAG mstaafu, Profesa Mussa Assad.
Katika kesi hiyo namba 01 ya mwaka 2019, Zitto anawakilishwa na wakili Nyaronyo Kicheere, anapinga Sheria ya Ukaguzi ya Taifa namba 11 ya mwaka 2008 inayoweka vipindi viwili vya mtu kushika wadhifa wa CAG.
Pia, anapinga uamuzi wa Profesa Assad kuondolewa katika wadhifa huo, akidai ameondolewa kabla ya muda wake wa utumishi kwa mujibu wa katiba. Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la majaji watatu Jaji Lameck Mlacha (kiongozi wa jopo), Jaji Benhajj Masoud na Jaji Juliana Masabo.
Waidaiwa katika Kesi hiyo ni Rais, AG na CAG Kichere akiwakilishwa na jopo la mawakili wa Serikali wanne, wakiongozwa na naibu Wakili Mkuu wa Serikali (DSG), Gabriel Malata na Profesa Assad anawakilishwa na jopo la mawakili wawili linaoongozwa na Ambros Mkwera, wameomba muda wa siku 14 kuwasilisha majibu. “Waheshimiwa majaji, kwanza tunakiri kwamba tumepokea maombi haya yaliyoko hapa mahakamani, Januari 23, 2020.”
“Pili tunakusudia ku-contest (kupinga) maombi haya kwa ku-file (kuwasilisha) reply (majibu ya hoja) na counter affidavit (kiapo kinzani) chini ya kanuni ya 6 ya kanuni za uendeshaji wa mashauri ya haki za Binadamu. Tunakusudia ku-file majibu yetu ndani ya siku 14 zilizotajwa kwenye hiyo kanuni,” amesema Malata.
Malata amefafanua kuwa kwa siku hizo wanapaswa kuwasilisha mahakamani majibu yao. Wakili Mkwera kwa niaba ya Profesa Assad naye amesema mteja wake anakusudia kuwasilisha kiapo kinzani dhidi ya hoja za mdai, na hivyo naye akaomba muda wa siku 14.
Mahakama imekubaliana na maombi ya mawakili hao na kuamuru kuwasilisha mahakamani hapo majibu yao, kwa muda huo waliouomba. Jaji Mlacha ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 18, 2020 itakapotajwa tena