Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 1:54 pm

NEWS:JOHN KIJAZI AWATAKA WAHANDISI WAZEMBE KUWAJIBISHWA

Dodoma: KATIBU Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ameitaka Bodi ya Usajili wa Wahandisi(ERB) kuchukua hatua kali kwa wahusika ambao wanaidhalilisha fani ya Taaluma yao kwa kufanya kazi chini ya kiwango.

Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma hapa wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya siku ya Wahandisi.

Katibu Mkuu huyo kiongozi amewakumbusha Bodi ya Usajili wa Wahandisi kuhusu umuhimu kutekeleza Mamlaka yake ya kisheria ya kuhakikisha kuwa taaluma ya Uhandisi inalindwa ipasavyo kwa kuiendeleza na kudhibiti ili ifanyike kwa utaalamu unaostahili.

“Sisi sote ni mashahidi wa baadhi ya barabara,madaraja,majengo ambayo yameharibika ndani ya muda mfupi sana tangu kujengwa na kusababisha hasara kubwa kwa Serikali na Nchi kwa ujumla

Balozi Kijazi amesema kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya Usajili wa Wakandarasi hadi kufikia Juni 2017 jumla ya Wakanadarasi 19,164 walikuwa wamesajili katika ngazi mbalimbali.

Amesema miongoni mwao 17,451 ni Watanzania na 1713 ni wa kigeni,hivyo Serikali inafanya jitihada za kipekee ili kuongeza idadi ya Wahandisi nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha elimu ya Sekondari na kuhamasisha vijana kusoma masomo ya Sayansi.

“Pamoja na kuwepo kwa fursa mbalimbali,jambo ambalo ninapenda kulisisitiza kwenu ni suala la kuwepo kwa utayari wenu na uwezo wenu katika kuzifikia na kufaidika na fursa,”alisema

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi,Prof.Ninatubu Lema,wameiomba Serikali kuelekeza miradi yote mikubwa na ile ya umma itumike kama madarasa ya wahandisi ili kupata utaalamu.

Pia amesema Makampuni yote ya nje yatakiwe kushirikiana na Makampuni ya ndani kwenye ujenzi na ushauri ili kukuza uwezo wa ndani.

Aidha amesema Serikali ipunguze na kupiga marufuku uingizaji wa bidhaana vifaa ambavyo vinaweza kutengenezwa hapa nchini.

“Mgeni rasmi tunayo nia ya kutaka kujenga jengo Mkoani Dodoma na kiwanja kimeishapatikana makisio yake ni kama Shilingi bilioni 10 tunawaka utaratibu wa kushirisha Wahandisi kuwa Patner kwenye mradi huo,’alisema