Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:42 am

NEWS:JESHI LA POLISI LANASA KILO 52 YA MILUNGI

Dodoma: JESHI la polisi mkoa wa Dodoma limefanikiwa kuwatia mbaroni watu wapatao wanne kwa makosa tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma,Lazaro Mambosasa,amesema tukio la kwanza lilitokea kijiji cha pandambili kata ya pandambili tarafa ya Mlali wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.

Aidha amesema mtuhumiwa mmoja aliyefahamika kwa jina la Hasan Ndossa (30) mkulima na mkazi wa Gairo mkoani Morogoro alikamatwa na gunia moja la mirungi lenye uzito wa kilo 52.

Amtuhumiwa huyo alikuwa akisafirisha mirungi hiyo kutoka wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro na kulekea wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili MC 975 BPE aina ya Haojue.

Mamba sasa alitaja matukio mengine kuwa ni baada ya kufanyika upekuzi uliofanyika kwenye nyumba ya Msafili Philimon (19) mkulima mkazi wa kijiji cha Kibakwe na Franck Mapembe (19) mkulina na mkazi wa kijiji cha Kibakwe

Amesema jeshi hilo lilikamata siraha aina ya Gobore 2,risasi aina ya chuma 70, zilizokuwa zikimilikiwa kinyum cha sheria,Radio tatu aina ya Mkulima,Betri moja ya Sola pamoja na simu 17 aina tofauti tofauti, viatu pea 12 aina ya boot, engo moja,kisu kimoja unga wa kutengenezea risasi chupa mbili.

Kutokana na taarifa za awali vitu hivyo vilipatikana kwa njia ambazo si halali na vimekuwa vikitumiaka katika matukio mbalimbali ya kiharifu.

Wakati huo huo jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limemfikisha mahakamani Omar Shemji (32) mkazi wa mbagala jijini Dar es Salama ambaye ni Dereva wa kampuni ya Mohamed Intreplise kwa kosa la kusababisha ajali iliyosababisha vifo vya watu wawili.

Ajali hiyo ilitokea Mei 2 mwaka huu majira ya saa mbili usiku eneo ha Ihumwa barabara kuu ya Dodoma Morogoro kata ya Nzunguni Manispaa ya Dodoma.

Amesema Lori yenye namba za usajili T191 CGX aina ya Faw na tela namba T851 ikiendeshwa na Omary Shemji aliigonga pikipiki yenye namba za usajili T 181 CXH aina ya toyoiliyokuwa ikiendeshwa na John Masuluali (41) mkazi wa Ihumwa mtaa wa chang’ombe mkulima na abiria wake Charles Mbwimbwi (42) mkulima mkazi wa Ihumwa mtaa wa Chang’ombe na kupelekea vifo vya wapanda pikipiki hao.

Katika matukio mengine Mambosasa amesema katika kijiji cha Kiseyu tarafa ya Kibaigwa wilayani kongwa Mkoani Dodoma simba wapatao 3 walivamia zizi la ng’ombe lililopo nyumbani kwa Juma Jonathan miaka (49)mfugaji na kuua ng’ombe 11.

Wananchi wa maeno hayo wametakiwa kuwa na taadhari na kuepukana kupta katika sehemu zenye vichaka kwani mpaka sasa haijulikani simba hao wako wapi ili waweze kurudishwa katika hifadhi ya wanyama ya Ruaha waikotoroka.