- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:CCM; YAWAKEMEA VIONGOZI WANAOJIFANYA MIUNGU WATU
Dodoma: chama cha mapinduzi (CCM) kimesema kuwa wakati wa baadhi ya viongozi kujifanya wakubwa kuliko wengine na kudharau wanachama kwa ubabe na jeuri umekwisha ambapo hali hiyo imesbabisha wanachama wengine kukihama chama hicho.
kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na naibu katibu mkuu wa CCM bara,Rodrick Mpogolo wakati akizungumza na viongozi,watendaji na wanachama wa ccm katika kikao maalum cha halmashauri kuu ya mkoa wa Dodoma.
aidha amebainisha kuwa wapo baadhi ya viongozi ambao wamedhulumu haki za wanachama kwa kuwashurutisha pamoja na kuwanyanyasa hivyo wanahitaji kubadilika.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi ndani ya chama hicho mpogolo amesema kuwa kila mwanachama ana haki ya kugombea na kuchagua kiongozi anayemtaka na ni mwiko kwa kiongozi kuweka maslahi binafsi mbele huku akipiga marufuku uwepo wa mawakala ndani ya chama
Kwa upande wao baadhi ya wanachama wa ccm wameelezea kuhusu ccm mpya ambayo ni ya mabadiliko waliyokuwa wakiyatamani kwa muda mrefu nawamekuwa na haya ya kusema.
Pamoja na hayo pia naibu katibu mkuu ametembelea na kukagua miradi mbalimbali iliyopo ndani ya manispaa ya dodoma ambapo amewataka viongozi kuisimamia kwa usahihi ili kuwanufaisha wanachama wote