Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:00 am

NEWS: ZOEZI LA VYETI FEKI KWA WATUMISHI WALIOGHUSHI BADO NITATA.

Dodoma: Serikali kupitia wizara ya utumishi wa umma na utawala bora imesema zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma bado unaendelea na kwa sasa wanaendelea kuhakiki wizara zote zilizosalia na kwamba matokeo ya uhakiki huo yatatolewa mei 10.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma Katibu mkuu wa utumishi Laurean Ndumbaro amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na kwamba awamu ya kwanza ilizihusisha idara zilizopo chini ya wizara ya utumishi wa umma pekee na kwa sasa zoezi hilo linaendelea kwa wizara zilizosalia.

Katibu mkuu ameendelea kusisitiza kuwa zoezi hilo halitawahusu wanasiasa na kuwataka wale wote ambao wanadai kuwa majina yao yametajwa kimakosa katika orodha iliyotolewa wiki iliyopita wapeleke malalamiko yao kwa waajiri wao pamoja na vielelezo vya uthibitisho kwa uhakiki zaidi.

Wakati hayo yakiendelea chama cha mawakili Tanganyika [TLS] kupitia baraza lake la uongozi limeazimia kumfungulia mashitaka mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa madai ya kughushi vyeti.

Siku chache Rais wa Tanzania John Magufuli alitangaza kuwafuta kazi watumishi wa umma elfu 9,932 kwa madai ya kutumia vyeti vya kughushi na kusema kuwa zoezi hilo ni endelevu huku akisisitiza kuwa zoezi hilo halitawahusu wanasiasa wakiwemo wakuu wa mikoa, wilaya, wabunge, mawaziri pamoja na madiwani.