- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO : ''SASA MBUNGE AKATAJE MAKOSA YA RAIS CHOONI''
KIGOMA: Mbunge wa jimbo la Kigoma Ujiji Mh. Zitto Kabwe amefuguka nakusema kuwa serikali ingeweza kununua ndege nyingine mpya iwapo ingeshughulikia vema kesi ya kampuni iliyoshikiria ndeye ya Bombadier Q400 ambayo Tanzania ilinunua.
Mh. Zitto ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa facebook
''Bei ya Ndege moja aina ya Bombadier Q400 ambazo Tanzania ina/menunua ni USD 31m. Deni tunalodaiwa pamoja na riba ambalo Serikali imekiri na kuahidi kulipa ni USD 37m.''alisema
''Hivyo Serikali yetu ingeweza kununua Ndege nyengine mpya iwapo ingeshughulikia vema kesi ya kampuni iliyoshikilia Ndege yetu. Hasara za namna hii ndio hurudisha nyuma Serikali za Afrika kwenye juhudi za Maendeleo''.
''Jambo la kushangaza ni pale Mbunge mwenye mamlaka ya Kikatiba kuihoji Serikali anapotimiza wajibu wake anakamatwa na kushtakiwa Kwa ' kutaja makosa ya Rais hadharani '. Sasa Mbunge ataje makosa ya Rais chooni? Chumbani? Shimoni? Mbunge wa Upinzani ni lazima ataje HADHARANI makosa ya Kiongozi wa Serikali ya Chama kinachoongoza dola''.alisema
''Kazi ya Upinzani ni kuhoji. Ni kazi ya kimantiki na ya kikatiba''alisema Zitto.
Kauli ya Zitto imekuja baada ya siku chache Mbunge wa Singida mashariki na mwanasheria mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo [CHADEMA] Tundu Lissu kukamatwa na jeshi la polisi kwa makosa mbalimbali likiwemo la kutaja makosa ya rais hadharani.
Ikumbukwe kuwa Kisa cha Lissu kuwekwa rumande ni pamoja na kuuliza maswali sita kupitia mtandao wake wa instragram siku chache kupita likiwemo suala la ndege aina ya bombadier ya Tanzania iliyonunua kuzuiliwa nchini canada.