- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO KABWE ARUDI TWITTER AANDIKA MAZITO JUU YA SEREKALI
Kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe leo amefanikiwa kurudi kwenye uwanja(platform ) wa kutolea maoni yake binafsi baada ya akauti hiyo kudukuliwa na watu wasiojulikana kwa kipindi cha takribani wiki kadhaa hivi.
Mara baada ya kurudi Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma mjini ameanza kwa kuwataarifu wafuasi wake kuwa amerudi hewa baada ya kukosekana kwa wiki kadhaa
"I am back on Twitter after weeks of absence due to forced take over of account by Tanzanian state agents following an abductio of my former Executive Assistant. Thanks @TwitterSupport for the swift action and this recovery. And what a day, my friend @kabsjourno imprisoned 5.8.19" aliandika zitto
''Walipopata access ya akaunti yangu waliweka tweets zao hizi. Tulikasirika kuwa wameingilia akaunti yangu lakini hizi ndio zilifanya tumwokoe Raphael. Pia hizi zinaonyesha kuwa mashabiki wa @MagufuliJP wanatafuta kuungwa mkono kwa nguvu kubwa''
''Walitaka pia kuleta mtafaruku ndani ya chama @ACTwazalendo ili kama kupunguza nguvu ya Chama katika kuhami demokrasia yetu na kuondoa udikteta unaonyemelea Nchi yetu.Nashukuru kuwa tupo imara mno ndani ya chama kwani tunajua shabaha yetu ni nini katika kuikoa Nchi yetu''
"Licha ya kuwa na magazeti na takribani vyombo vyote vya habari kuwekwa chini yao bado wanatafuta kuungwa mkono. Hii ni dalili kuwa hawana la kuonyesha kwa Umma hususan baada ya Ripoti ya TISS kuonyesha kuwa Rais @MagufuliJP hawezi kushinda Uchaguzi huru na haki 2020''
"Walijaribu kutaka kuonyesha kuwa miradi ya Maendeleo inayotekelezwa Kigoma ni yao . Sio kweli. Miradi yote ya Maendeleo Kigoma ni juhudi zetu wenyewe kama Manispaa ya @KigomaUjijiMC na miradi mingi Serikali ya @MagufuliJP imekwamisha ili kutukomesha, eg Luiche Irrigation scheme" aliandika Zitto
"Siwezi kuunga mkono Serikali inayoteka watu, inayoua watu, inayofunga watu jela kwa makosa ya kubumba, inayoua demokrasia ya vyama vingi na muhimu zaidi inayoua Uchumi wa Nchi yetu. Watanzania sio wajinga na ndio maana Rais Magufuli amekuwa Rais anayechukiwa na wananchi zaidi"