- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO AZITILIA MASHAKA TAKWIMU BAJETI YA WAZIRI MPANGO
Dar es salaam: Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa kuna mashaka makubwa katika takwimu zinazo tolewa na serikali kuhusu ukuaji wa pato la taifa na la mtu mmoja mmoja(Per capital income) .
Amesema, takwimu zilizotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango, Bungeni Juzi wakati wa kuwasilisha Makadirio na Mapato kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 kwamba, uchumi umekuwa kwa asilimia 7, zina mashaka kulinganisha na takwimu zingine za serikali.
Maelezo hayoZitto ameyasema jana tarehe 16 Juni 2019, wakati akifanya uchambua wa bajeti ya mwaka ya taifa kwa mwaka 2019/20 mbela ya wanahabari Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
“Kuna mashaka makubwa na kasi ya ukuaji wa mapato ya serikali, tumejaribu kuangalia miaka iliyopita, yaani mwaka 2013/14, 2014/15, 2015/16, 2016/17, 2017/18 na 2018/19, tunaona kasi ya ukuaji wa mapato imeshuka mpaka asilimia 2. Kwa hiyo ukisema serikali inaongeza mapato, ni ulaghai mtupu, ni uongo.
“Na sasa hivi utaona ndio maana wanakutana na wafanyabiashara, wanawafurahisha furahisha kwasababu wamegundua mapato yameshuka, na haya ni matokeo ya maamuzi ya kwanza kwenye bajeti ya kwanza ya serikali hii,” amesema Zitto.
Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo, ameeleza kushangazwa na kauli ya serikali kwamba, pato la taifa linakuwa kwa asilimia saba na kuwa, mwaka jana lilikuwa asilimia 6.8. “Tumefanya marejeo. Tunatilia mashaka hizi takwimu. Hesabu za Benki ya Dunia zinaonesha ukuaji ni wa asilimia sita.
Hesabu za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) zinaonesha ni asilimia 4.2 kwa mwaka huu 2019, lakini mwaka jana kwenye asilimia 5 hivi,” amesema.
Akieleza sababu za mashaka hayo amesema, uchambuzi wao umekuja na hoja mbili ambazo ni takwimu zilizopo kwenye kitabu cha serikali kinachoitwa ‘Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa’ katika mwaka husika, na pili ni mtiririko wa kipato cha mtu mmoja mmoja kuanzia mwaka 2014.