Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:37 pm

NEWS: ZITTO ATAKA WACHUNGUZI WA KIMATAIFA KWENYE SHAMBULIO LA LISSU

Dodoma: Mbunge wa kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe amehitaji kufanyika kwa uchunguzi kutoka mataifa ya njee juu ya shambulio la kupigwa Risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, akiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Zitto amesema kuwa vyombo vya ndani ya nchi hatuviamini tena"I call for an independent INTERNATIONAL investigation on assassination attempt against MP Tundu Lissu. Local organs shall not be trusted." alisema Zitto

Zitto amesema kuwa waliomshambulia Lissu wanampango wa kututisha tusiseme frikra zetu na kusema kuwa kama kweli watu watakaa kimya watakuwa wameshinda


"Lissu attackers aim at threatening us to speak our minds. If we keep quiet, they win"


Zitto alimalizia kwa kusema kuwa hatuwezi kuwapa nafasi hiyo ya kukaa kimya tunaongea kuhusu HAKI. ''We shall not give them that. Speak against injustices''

Lissu alishambuliwa kwa Risasi na watu wasiojulikana siku ya Alhamisi ya Tarehe 7 septemba mwaka huu nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma akitokea kwenye shughuli zake za kikazi. na kwasasa yupo Jijini Nairobi kwa matibabu zaidi katika Hospitali ya Aga Khan