- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO ASEMA YUKO TAYARI KUGOMBEA URAIS 2020
Dar es Salaam. Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo , Zitto Kabwe amesema atakuwa tayari kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020 endapo vyama watakavyoshirikiana navyo katika mchakato huo vitaridhia.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini ametangaza msimamo huyo leo Jumanne, Desemba 31,2019 wakati akitoa salamu za mwaka mpya za ACT- Wazalendo akiwa na Mshauri mkuu wa Chama hicho Maalim Seif huku akiwapa pole wananchi waliofikwa na changamoto mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2019.
Zitto amefafanua kuwa hivi sasa sio suala nani anafaa kugombea bali ni mchakato wa wadau na vyama vya siasa kukaa chini pamoja kuangalia namna ya kukiondoa chama tawala cha CCM.
Zitto amesema baada ya wadau na vyama vya siasa kukaa pamoja kinachofuata ni kuangalia kuwa kutokana na changamoto zilizopo fulani anafaa kugombea kiti cha urais.
"Suala siyo mimi kugombea bali ni mazingira na muktadha. Kwa wenzangu wakisema kulingana na mazingira haya Zitto anafaa kugombea sitokimbia msalaba huu,β amesema Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini.
Alipoulizwa kuhusu kutogombea ubunge iwapo atagombea urais, Zitto amesema, "suala la hapa sio nauweka ubunge wangu rehani hapana. Unapokuwa kwenye mapambano lazima uwe tayari kwa lolote."