- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO ASEMA MAALIM SEIF KUHAMIA ACT HAUKUWA MPANGO WA GHAFLA
Dar es salaam: Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, amesema uamuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (Cuf), Maalim Seif Sharif Hamad wa kuhamia ACT haukuwa wa ghafla bali ulikuwa na mchakato.
Zitto ametoa kauli hiyo leo Machi 20, 2019 wakati akihojiwa katika kipindi maalumu cha Kwanza TV, Zitto amesema pamoja na kwamba ilikuwa ni mchakato wa maandalizi wa kwao (kina Maalim Seif) na wao (ACT) walijiandaa kwa lolote, kwani kwa muda mrefu walikuwa wanasisitiza katiba ifuatwe.
“Watu wasidhani mambo haya ni maandalizi ya muda mchache baada ya hukumu, bali ni maandalizi ya muda mrefu ya kujenga imani kujiandaa kisaikolojia na si ACT pekee bali vyama vyote na watu wanaopenda mabadiliko na wamechoshwa na kuburuzwa ndani ya CCM.
“Ilikuwa Maalim akoseshwe jukwaa ili ashindwe, Ni lazima juhudi za mapambano ya kudai demokrasia ziendelee na kuungana na wenzetu ambao hawakutendewa haki ili waweze kuendelea na mapambano,” amesema Zitto.