Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 10:30 am

NEWS: ZITTO AMTAKA SPIKA WA BUNGE KUMCHUKULIA HATUA RC MAKONDA

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amehoji kauli iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda dhidi ya Wabunge, akidai kuwa inalidhalilisha Bunge hivyo amemuomba Spika wa Bunge Job Ndugai kutoa muongozo juu ya kauli hiyo.

Image result for zitto na spika ndugai

Zitto alitoa kauli hiyo leo Juni 25, 2019 Bungeni Jijini Dodoma baada ya Ndugai mapema kabla ya kuhuruhu wabunge kuanza kupiga kura kupitisha bajeti ya Serikali mwaka 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni, kusema kati ya wabunge waliokwenda Misri ambako timu ya Taifa inashiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), hakuna aliyemlaumu mchezaji yeyote wala kuisema vibaya timu hiyo.

Baada ya kauli hiyo Zitto aliomba mwongozo, “Kwa mujibu wa kanuni ya 68 (7) kuhusu jambo lililotokea bungeni mapema naomba kupata ufafanuzi wako, muda mfupi uliopita umeeleza jambo lililotokea nje ya Bunge ambapo mmoja wa viongozi wa Serikali mbele ya kiongozi mkuu wa nchi amewabagaza wabunge ukiwemo wewe mwenyewe.”

“Lakini maelezo uliyotoa utadhani sio mkuu wa mhimili, umetoa maelezo kama unajitetea mbele ya kiongozi huyo kitu ambacho nadhani Spika tunapaswa kupata mwongozo wako, maana atatokea mwingine atawasema wabunge na hakutakuwa na chochote cha kufanywa,” amesema Zitto.

Ameongeza, “Wewe hauruhusu mhimili wa Bunge kuchezewa, kutomaswa na kudharauliwa nini kilichokupata leo unasamehe kabla ya kuchukua hatua yoyote. Simama kulinda hadhi ya Bunge na wabunge hawajawasema wachezaji "

Katika majibu yake Ndugai amesema, “Hayo ni mawazo ya mtu ambaye kidogo ndio hivyo.

Ni bahati mbaya sana tuna viongozi wa Serikali wanadiriki kumdanganya Rais hadharani, kiongozi wa Serikali unapoongea mbele ya rais jipange uongea ukweli mtupu wa mwenyezi Mungu, usisingizie wala kumuonea mtu hatufanyi hivyo.” “Natamani ningefunguka kidogo kuhusu…,

bahati mbaya kijana wetu huyu hajitambui na hajielewi na kwa sababu ana nguvu aliyonayo ana makundi ya vijana kwenye mitandao anaweza kumtukana Spika, kuwasingizia wabunge wamekosa nini? Kama kuna mtu ana deni la kufanya kidogo kuhusu hao wachezaji basi ni yeye. Akitaka niseme ila kwa leo inatosha.”

Mapema leo asubuhi, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika ufunguzi wa Mradi wa Gesi, Kigamboni jijini humo, alisema ameshangaa wadau mbalimbali ambao wameizungumzia vibaya timu hiyo baada ya kupoteza mbele ya Senegal.

"Nimeumizwa na matokeo ya Taifa Stars, lakini nimeumizwa zaidi kwa watu kuwabeza wachezaji wetu ambao wametubeba watanzania ambao ndani ya miaka 30, haikuwezekana lakini wao wamepambana mpaka tupo Afcon leo hii," alisema Makonda

Makonda alisema alizungumza na wachezaji hao pamoja na nahodha Mbwana Samatta na wamemuhakikishia kwamba watafanya vizuri katika mchezo wao dhidi ya Kenya. "Sisi Afrika Mashariki tunajuana vizuri kwahiyo Mhesimiwa Rais wala usiwe na wasiwasi tutafanya vizuri katika mchezo huu ambao tunahitaji ushindi na wachezaji wapo vizuri," alisema Makonda.