- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO AMJIBU SPIKA NDUGAI DHIDI YA MKOPO WA BENKI YA DUNIA
Dar es Salaam. Kiongozi Mkuu wa chama cha (ACT-Wazalendo) nchini Tanzania, Zitto Kabwe ameikosoa vikali kauli ya Spika wa Bunge, wa Tanzania Job Ndugai aliyehoji kwanini Zitto aliindikia barua Benki ya Dunia (WB) akitaka Tanzania inyimwe mkopo wa miradi ya elimu.
Zitto amesema hakuna tofauti ya kisera katika suala la watoto wa kike wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.
Ndugai ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Januari 31, 2020 bungeni mjini Dodoma baada ya maelezo ya naibu waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara aliyekuwa akijibu swali la Mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul aliyetaka Serikali iingize suala la ujenzi wa nyumba za walimu katika bajeti.
Akizungumza baada ya majibu ya Waziri Waitara, Ndugai amesema Zitto kuandika barua hiyo ni tofauti za kisera, lakini kuzuia fedha za Benki ya Dunia ni kwenda mbali zaidi.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Zitto ambaye yupo nchini Canada amesema, “hakuna tofauti ya kisera katika suala la watoto wa kike wanaopata ujauzito kuendelea na masomo. Ilani ya CCM iliahidi hilo, wananchi mwaka 2015, vyama vya Upinzani viliahidi hilo na wananchi 2/3 wanaunga mkono hilo.”
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma mjini ACT Wazalendo, amesema hata ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 inataka watoto wa kike waliopata ujauzito warudi shuleni.
“Asilimia 71 ya wananchi wanaunga mkono watoto wa kike waliopata ujauzito kuendelea na masomo. Ilani ya CCM pia inataka warudi shule,” amesema.