- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO ALAANI KITENDO CHA JAMHURI KUTAKA HATI YA KUKAMATWA LISSU
Mbunge wa Kigoma Mjini zitto Kabwe amelaani kitendo cha Jamhuri ya Tanzania kuiomba Mahakama kutoa hati ya kukamatwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
Zitto amesema Lissu yupo Kitandani baada ya kufanyiwa Operesheni zaidi ya Ishirini mwilini mwake huku akiongezea kwa kusema kuwa kitendo hicho sio cha Utanzania
"Serikali KATILI imegomewa na mahakama kufanya kitendo cha kishenzi cha kutaka kumkamata mgonjwa. Tundu Lissu yupo kitandani baada ya operesheni ya ishirini na ngapi sijui, bila aibu Serikali inataka hati ya kumkamata Eti haji mahakamani.Huu sio Utanzania kabisa." ameandika Zitto kupitia mtandao wake wa Twitter
Wakili wa Serikali, Simon Wankyo Leo Jumatatu aliwasilisha maombi akiitaka Mahakama hiyo itoe hati ya kumkamata Mbunge huyo katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge huyo na wahariri wa gazeti wa la Mawio, Wankyo amedai mshtakiwa anaonekana akizunguka nchi mbalimbali akitoa mihadhara na huko Ubelgiji anakodaiwa yuko Hospitali haijaelezwa yuko hospitali gani.
Lakini Hakimu Mkazi Mkuu, wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ameyakataa maombi hayo ya upande wa Jamhuri katika kesi hiyo ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa huyo wa Singida Mashariki na wahariri wa gazeti wa la Mawio.
Lakini Hakimu Simba amewataka wadhamini wa Lissu ambao ni Ibrahim Ahmed na Robert Katula kuhakikisha wanahudhuria mahakamani hapo kila kesi hiyo inapokuwa Inatajwa. Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 25, Mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Kesi hiyo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa mashtaka, lakini imeshindwa kuendelea kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, ( Lissu )kuwa nchini Ubeljiji kwa ajili ya matibabu.
Mbali na Lissu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni wahariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh. Kwa pamoja washtakiwa hao, wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.
Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati Januari 12 na 14, 2016 jijini Dar es Salaam, ambapo Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’