Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:23 am

NEWS: ZITTO AIJIA JUU SEREKALI TENA, JUU YA KUFUNGIWA KWA MAGAZETI

Dar es salaam: Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amelaani kitendo cha Serekali kulifungia gazeti la Raia Mwema September 27, mwaka huu na kusema kuwa Serekali ya awamu hii inaongoza kwa kufungia magazeti kuliko serekali zilizowahi kuongoza tangu kupata uhuru mwaka 1961

"Serikali ya CCM ya Awamu ya 5 inaongoza kufungia magazeti kuliko Serikali zote zilizopita.

Zitto anasema kuwa hakuna sababu za msingi za kulifungia gaziti la Raia mwema kwa sababu gaziti hilo linafanya ukosoaji wenye staha "Sababu za Kufungia gazeti la RaiaMwema hazina msingi wowote na ni aibu kubwa."
"Ukosoaji unaofanywa na RaiaMwema ni ukosoaji wenye staha unaopaswa kulindwa kwenye jamii yeyote yenye kuheshimu demokrasia.

''Kama hutaki kukosolewa huna sifa ya kuwa Kiongozi wa Umma, tena kwenye Nchi ya wastaarabu Kama Tanzania." aliandika zitto Kwenye ukurasa wake wa facebook.

Kumekuwa na wimbi la kufungia vyombo vya habari nchini Tanzania kwa tuhuma mbalimbali kama za kufanya uchochezi, kumkashifu Rais, na zinginezo, baadhi ya magazeti ambayo yamewahi kufungiwa ni Mawio, mwanahalisi awamu ya kwanza, mwananchi na mtanzania septemba 27 2013, Mwanahalisi na Raia mwema ya tarehe 28 septemba mwaka huu.