- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO AIJIA JUU SEREKALI BAADA YA KUTUHUMIWA KUHUJUMU NCHI
Dar es salaam: Mbunge wa kigoma Ujiji na Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi kabwe ameilaani kauli ya Kaimu Msemaji mkuu wa Serekali Zamaradi kawawa kuwa wanasiasa ndio Wanashirikiana na kampuni za njee kuhujumu nchi "Hakuna mwanasiasa anayeweza kushirikiana na kampuni za kigeni kuhujumu nchi. Mimi binafsi filosofia yangu ni rahisi Sana ' My Country, Right or Wrong '. Maneno yanayosambazwa kuwa nimeshiriki kuwezesha Ndege ya Bombardier iliyonunuliwa na Serikali Kwa niaba ya ATCL kukamatwa huko Canada ni takataka tu zinazosambazwa na wapika propaganda."
Kitendo cha Msemaji wa Serikali kulaumu wanasiasa Kwa jambo la kisheria Kama hili ni utoto." Alisema Zitto "Serikali lazima ifahamu kuwa ni lazima ihojiwe na iwe tayari kutoa majibu. Sisi kama vyama vilivyo Nje ya Serikali Ni wajibu wetu kuhoji jambo lolote. Pia ni haki yetu kupata Taarifa zozote kutoka mahala popote zitakazosaidia kuisimamia Serikali. Wajibu wa Serikali ni kujibu hoja zinazoibuliwa. Majibu ya Msemaji wa Serikali yanataka kuligeuza suala hili kuwa la kisiasa na watu wameangukia kwenye ushabiki huo. Hili ni suala la kisheria na suala la nchi ambayo sisi wote tuna maslahi ya kuona inakwenda mbele"
Nchi kudaiwa sio dhambi. Hata mataifa makubwa duniani yanadaiwa. Watu binafsi tunadaiwa sembuse Serikali? Mimi ninadaiwa madeni ya uchaguzi mpaka Sasa na wengine wamenipeleka mahakamani. Sio dhambi kudaiwa. Muhimu ni 1) Deni limetokana na Nini? Ni maamuzi mabovu ya kisiasa? 2) unalipa deni hilo au kuweka mikakati ya kulipa? Aliongea Zitto
Hii ni nchi yetu sote. Hakuna mwenye hatimiliki ya ukweli. Ukweli pia haupendi kupindwa pindwa. Serikali itoke kueleza nini kimetokea mpaka Ndege kuzuiwa, iachane na tabia ya hovyo ya kutafuta mchawi ' kwamba eti wanasiasa Ndio wamesababisha '. Kutafuta mchawi ni kutowajibika Kwa maamuzi ya Serikali yenyewe. alimalizia Zitto