Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:36 pm

NEWS: ZITTO AHOJI MASWALI NONDO BUNGENI

Dodoma: Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), ambaye pia ni Kiongozi mkuu wa chama Zitto Kabwe amehoji Juu ya Mwenendo wa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DDP) kufanya makubaliano na baadhi ya washtakiwa kulipa kiasi fulani cha Pesa ili kupunguziwa adhabu au kufutiwa mashtaka na kuhoji fedha wanazolipa washtakiwa hao zinakwenda wapi na nani anazikagua pesa hizo.

"Tunatengeneza a 'ganster's republic' kwamba dola inamkamata mtu, inamwamuru toa hela kama hutaki kutoa hela huwezi kutoka...! "Twambieni hizi fedha zote mabilioni alizokusanya DPP zimekwenda wapi? Nani anazikagua maana hatuzioni kwenye vitabu!" anahoji Zitto Kabwe

Kauli hizo za Zitto amehoji jana jioni Aprili 12, 2019 wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora) ni hesabu za Takukuru kutokaguliwa pamoja na Wakala wa Ndege za Serikali kuhamishiwa ofisi ya Rais.

“Kumekuwa na utamaduni ofisi ya mwendesha mashtaka kukamata watu, hatujui kama wanabambikiwa kesi au la, lakini baadaye tunaona watu wale wanakubaliana na ofisi ya DPP na kulipa pesa na kesi hiyo inakwisha,” amesema Zitto.

“Ningependa nchi yetu ipate ufafanuzi huenda kuna uonevu mkubwa sana, kwamba watu wanabambikiwa kesi kwa utakatishaji fedha wanawekwa ndani ili wazungumze na DPP halafu waende mahakamani wakiri na kulipa faini kiwango ambacho wameshtakiwa nacho.”

"Tumetumia zaidi ya 1T kununua ndege, lakini mchakato huo wa manunuzi umefanywa kwa Siri, hakuna anayejua tumenunua vipi, na CAG hajakagua. Ghafla tunaambiwa Wakala wa Ndege za Serikali ambao Ndio wamiliki wa Ndege 6 za ATCL sasa Upo Ofisi ya Rais Fungu 20" amehoji Mbunge Zitto Kabwe